WAMILIKI wa magari wametakiwa kufuata sheria ya kuyaondoa barabarani magari yao yanayopata ajali ndani ya saa sita.
Kauli
hiyo ilitolewa bungeni jana na Naibu Waziri wa Ujenzi, Gerson Lwenge
wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Al-Shaymaa Kwegyir (CCM).
Katika swali lake, Kwegyir alitaka Serikali kutunga sheria ya
kuwawajibisha
wamiliki wa magari yanayopata ajali kulipa gharama za kunyanyua magari
yao badala ya kuwatumia askari wa usalama barabarani.
Mbunge
huyo pia alitaka kujua kama ipo bei elekezi inayotumika kuwaongoza
wamiliki wa winchi kwa kazi ya unyanyuaji wa magari yanayopata ajali.
Lwenge
alisema gari linapopta ajali ni wajibu wa mmiliki kuhakikisha anaondoa
gari lake mapema iwezekanavyo ili kutokuwa na kizuizi cha kufunga
barabara.
Alisema
Sheria ya Barabara namba 13 ya mwaka 2007 inaeleza kuwa gari lolote
linaloharibika barabarani linatakiwa kuondolewa na mmiliki.
“Hakuna
bei elekezi ya kuwaongoza wamiliki wa winchi kwa kazi ya unyanyuaji wa
magari yaliyopata ajali bali kinachofanyika ni maelewano kati ya mwenye
winchi na mmliki wa gari lililopata ajali,” alisema.
Alisema
sheria hiyo inaeleza wazi kuwa endapo wamiliki wa magari yanayopata
ajali barabarani watachelewa kuita winchi la kuoliondoa gari ndani ya
barabara, mamlaka ya barabara italiondoa gari hilo na wamiliki
wanawajibika kulipa gharama zilizotumika.
Lwenge alisema mbali na kulipa gharama hizo pia mmiliki atatakiwa kulipa faini zitakazoamuliwa kwa mujibu wa Sheria ya Barabara.
No comments:
Post a Comment