Pages

Tuesday, June 30, 2015

SHABAN KISIGA AJIUNGA NA RUVU SHOOTIG



Aliyekuwa mshambuliaji wa Simba, Shaban Kisiga (pichani) amejiunga na klabu ya Maafande wa Ruvu Shooting kwa mkataba wa mwaka mmoja ili kuinusuru kuirejesha ligi kuu.

Kisiga aliondoka Simba baada ya kutokea sintofahamu na uongozi wa klabu hiyo, hasa benchi la ufundi na kuamua kutimkia kusikojulikana.



Akizungumza na Habari Maseto Ofisa habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire alisema, nyota huyo amemwaga wino wa mwaka mmoja, na kutokana na uwezo wake dimbani ndio sababu ya kumnyakua.

No comments:

Post a Comment