Na Woinde Shizza, libeneke la kaskazini blog
Mwendesha magari Randeep Shingh kutoka jijini Dar es Salam
ameibuka mshindi katika mashindano ya
kila mwaka ya mbio za nyika za
magari nane-nane rally yaliyotimua vumbi
katika mji wa Arusha mwishoni mwa wiki.
Mashindano hayo yamefanykia kwa siku mbili mfululizo huku
yakishuhudiwa ushindani mkali kwa madereva hao waliotoka mikoa mbalimbali na
Randeep Shingh akiwa na msoma ramani Guvinder Singh wa gari ya Mitsubishi
lancer akiibuka mshindi wa jumla katika mashindano hayo.
Katika mashindano hayo yaliyokuwa yakitofauti mwaka huu,
baada ya kufungiwa mitambo ya kisasa ya kidigitali kwa kila gari ili kuwezesha
ufuatiliwaji wa kila gari na njia zitakazopitia kwa ajili ya kuhakikisha kuwa
hakuna zengwe wala suala la madereva kuiba njia
na hata kupotea porini.
Zaidi ya madereva 20
kutoka ndani na nje ya nchi
walioshindana zaidi ya Km 198
huku mshindi wa pili akiwa ni Raj Pal
Dhani na msoma raman Sinder Sudle
wakiwana na ghari la Subaru Impreza nafasi ya tatu ikiwa imeshikwa na
Gurjit Singh huku dereva mkongwe wa
nchini Tanzania, Gerald Miller akiambulia nafasi ya sita, HUKU baadhi ya madereva walioshiriki
katika mashindano hayo wakisema yalikuwa magumu mwaka huu huku wengine
wakizungumzia changamoto ya barabara, baadhi ya mashabiki wa mchezo
waliojitokeza kwa wingi kutazama mashindano ya hayo ya Utrack nanenane rally walisema wamefurahi na
kuiomba serikali kuwezesha mashindano haya kufanyika mara kwa mara
No comments:
Post a Comment