Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, July 31, 2015

HOT NEWSS::HII NDIO BARUA KUTOKA BASATA KUMFUNGIA MSANII SHILOLE KOTOFANYA MUZIKI KWA MWAKA MMOJA

 http://i.ytimg.com/vi/eMup7g-uOUM/maxresdefault.jpg

Tarehe 9 May 2015 ukiwa katika onyesho lako la muziki Ubelgiji ulicheza uchi mbele ya hadhira ya wapenda sanaa za Tanzania hivyo kudhalilisha utu wako na jamii ya kitanzania kimaadili

BASATA ilipata habari zako, kumbuka pia October 2013 BASATA lilikuonya na ukakiri kwa kuomba msamaha tabia yako ya kucheza bila kuzingatia maadili uwapo jukwaani, BASATA ilikupa nafasi ya kutoa maelezo kwanini usichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kitendo chako lakini umekaidi kutoa maelezo yako‘ – BASATA
Shilole 
Baraza limejiridhisha kwamba ulikiuka maadili ya kazi ya sanaa kwenye onyesho lako huko Ubelgiji makusudi na umekiuka sheria kwenye ibara ya 30 (2) ya katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kwa kuvunja maadili ya jamii ya Mtanzania hivyo baraza linakusimamisha 

 
kujishughulisha na kazi za sanaa nchini na nje ya nchi kwa mwaka mmoja, kufanya kinyume na hayo kutapelekea kupewa adhabu zaidi pamoja na yeyote utakaeshirikiana nae ‘ – BASATA



TABU
TABO 2

No comments:

Post a Comment