Pages

Thursday, July 2, 2015

KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI WAFANYA UKAGUZI WA KUSHTUKIZA KITUO CHA MABASI UBUNGO


Kikosi cha usalama barabarani chafanya ukaguzi wa kushtukiza katika kituo cha mabasi Ubungo.
Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani kimefanya ukaguzi wa kushtukiza katika kituo kikuu cha mabasi Ubungo ambapo baadhi ya  magari yamekutwa na mapungufu mbalimbali ikiwepo kufunga spring kwa kutumia kamba za katani, minyororo na manati huku baadhi ya vipuri muhimu vikiwa vimeegeshwa juu kwa juu ili mradi liende hatua ambayo inahatarisha usalama wa abiria.

 
ITV ilifika kituoni hapo na kushuhudia ukaguzi huo ukifanyika kwa umakini mkubwa tofauti za siku za awali ambapo askari hao walikuwa wakiingia chini ya uvungu wa gari na kubainisha mapungufu hayo ambapo baadhi ya abiria wameuzungumzia.
Aidha baadhi ya wasimamizi wa magari ambayo yamekutwa na mapungufu wamesema ukaguzi kama huo hata wao unawarahisishia kwa mabosi wao kwani mara nyingine walikuwa wakisema kuwa gari ni bovu wamilki wamekuwa wanakuwa ni wagumu kuelewa.
Hata hivyo baadhi ya wamiliki wa magari walokuwa kituoni hapo kushuhudia zoezi hilo wamekiri magari yao kukutwa na makosa
na kuahidi kuwa watahakikisha wanaongeza umakini katika kuyatunza magari yao ili kupunguza ajali zisizokuwa na sababu.
Kamanda Mohamedi Mpinga ni mkuu wa kikosi cha usalama barabarani ambaye amesema amegundua kwa siku za awali ukaguzi ulikuwa unafayika pale Ubungo ulikuwa haukidhi mahitaji halisi na hivyo  amepeleka timu mpya ili kupunguza kero na malamiko ya mara kwa mara pamoja na kuanisha mambo ambayo yamebainika katika ukaguzi huo.

No comments:

Post a Comment