Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, July 29, 2015

SHILOLE KIUNO, NUH MZIWANDA WAPATANISHWA KWA KAJALA


Imelda Mtema
BAADA ya kujinadi kwa mbwembwe nyingi mitandaoni kuwa wamemwagana, hatimaye wapendanao, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ na Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ wamepatanishwa na kufungua ukurasa mpya wa ‘malovee’, Risasi Mchanganyiko linakumegea.
Chanzo kilicho karibu na wawili hao kilipenyeza habari kuwa, Shilole na Nuh Mziwanda walilazimika kupatana baada ya kukutanishwa kwenye bethidei ya Kajala bila kujijua na kuombwa wapatane.
“Kwani hamjui kuwa walipatana siku ile ya bethidei ya Kajala? Kama hamuamini muulizeni Kajala atawapa ubuyu kamili lakini habari ndiyo hiyo, walikutana, wakakumbatiana na kuanza upya,” kilisema chanzo chetu.

Baada ya kunyaka ‘ubuyu’ huo, mwanahabari wetu kwa kutumia vyanzo mbalimbali alifanikiwa kuzipata picha za Shilole na Nuh wakiwa wamekumbatiana kwenye sherehe hiyo iliyofanyika nyumbani kwake, Afrikasana jijini Dar.



Mwanahabari wetu alimvutia waya Kajala ili aweze kuzungumzia tukio hilo ambapo alisema aliamua kuwapatanisha kwa sababu anapenda ‘kapo’ yao hivyo kitendo cha wawili hao kutokuwa pamoja kilikuwa kikimuumiza moyo.


Hata hivyo, baada ya kupatanishwa, wadau wa burudani Bongo ambao hawakupenda majina yao yaandikwe gazetini, waliwaonya wawili hao kutulia na iwe mwisho kugombana maana si mara ya kwanza kugombana.
Kabla ya kupatanishwa, wawili hao walikuwa wakitupiana madongo mitandaoni wakionesha kuwa hawana dalili za kurudiana lakini hatimaye wamekubaliana kuwa pamoja kwa mara nyingine.

No comments:

Post a Comment