Na Waandishi Wetu
Dar/Mikoani. Baadhi ya wabunge wa Chadema wanaotetea viti
vyao wameibuka kidedea katika kura za maoni zilizofanyika katika majimbo
mbalimbali nchini jana.
Hao ni pamoja na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi
‘Sugu’ aliyejizolea ushindi mnono wa kura 356 akiwaacha kwa mbali wapinzani
wake, Joyce Mashine aliyepata kura43 na Tito Mwanjale kura 18. Wengine
waliokuwa wakiwania kuteuliwa na chama hicho ni Lazaro Mwankemwa aliyepata kura
15, Christopher Nyenyembe (12) na Sishe Simbeye (6).
Mbunge mwingine, aliyepata ushindi wa kishindo ni Highness
Kiwia wa Ilemela aliyejizolea kura 134 na aliyemfuatia alikuwa Gasper
Mwanaliela ambaye alipata kura 28.
Wabunge wengine, Joshua Nassari hakuwa na mpinzani katika
Jimbo la Arumeru Mashariki kama ilivyokuwa kwa David Silinde katika Jimbo la
Momba.
Tafrani Mbeya Mjini, Mbarali
Awali, kulizuka tafrani iliyotokana na mgombea, Meshack
Kapange kuenguliwa. Mgombea huyo alipinga akidai kuwa hakutendewa haki na
kwamba kilichofanyika ni kumkingia kifua Sugu.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Chadema Mbeya Mjini, John
Mwambigita alisema Kapange alikwishavuliwa uanachama na suala la kuchukua fomu
za kuomba ubunge ilikuwa ni haki ya kila mmoja.
Kapange alisema atakata rufaa kwa kuwa hakutendewa haki na
wasimamizi wa mchakato huo... “Nimempigia Katibu Mkuu wa Chadema (Dk Willibrod
Slaa), akaniambia yuko kwenye mkutano Mwanza, nitampigia kesho (leo) kumweleza
kunyang’anywa haki yangu,” alisema. Mzozo mwingine uliibuka Mjini Mbarali baada
ya Jidawaya Kazamoyo aliyepata kura 109 kulalamika kuwa ndiye mshindi na kuzuka
vurugu zilizosababisha Liberatus Mwang’ombe aliyeshinda kwa tofauti ya kura
moja kutolewa nje ya ukumbi akiwa chini ya ulinzi mkali.
Matokeo ya kura ya maoni Chadema
Segerea: Anatropia Theonest (49), Kisheli Mchele 26 Masato
Wasira (24), Baraka Sawema (15), Habron Mwakagenda (6), Bakari Yusuph (2),
Loyce Gibona (2), Amos Maziku (0), Dominic Orembe (0), George Martin (0).
Lupa: Miraji Hussein amepata kura (65) na kuwashinda wenzake
Njelu Kasaka (45) na Fillipo Mwakibinga (32).
Korogwe Mjini: Amani Kimea amewashinda kwa mbali wenzake
watano kwa kupata kura 56. Aliyefuata ni Mwakolo Wynjones (26), Calistus
Shekibaha (8), Steven Kimea (4), Benson Mramba (1) na Grayson Kibwana (0).
Busega: David Nicad (116), Buluba Mabelele (67), Revocatus
Madundo (55), Modest Masunga (4), Sajda Dotto (3), Mapambano Ochalo (2),
Keneddy Lufulondama (1), Adam Komanya (0), Lutandula Mabimbi (0) na Mhere Mwita
(0).
Sikonge: Godfrey Ndaki (16), Moses Kaombwe (17), Dk Mmeta
Yongolo (19), Mtemi Zombwe (70) na Hija Ramadhani 83.
Manyoni: Alute Emmanuel (171) na Thedey Meremeta (47)
Vwawa: Fanuel Mkisi (136), Stephen Mwamengo (42), Solomon
Kibona (22), Andrea Bukuku (9), Fadhil Shombe (8), Bob Mwampashe (5) na
Jonathan Mwashilindi (5).
Ilemela: Highness Kiwia (134), Gasper Mwanaliela (28),
Bugumba Nsumba (20), Wema Dilala (17), Deus Ng’hanyanga (15), Edwin Sarungi
(13), Telexphone Masalu (8), Kageshiza Mwendesha (7), Mayalo Kasili (3),
Thobias Mogole (7), Magesa Masinde (6), Damas Kimenyi (5), Habath Matalu (5),
Greyson Wanzagi (13), Darius Ngocho (5), Humphrey Mmanda (3), Malehe Sweta (3)
na Frederick Mataja (2).
Mbozi: Paschal Haonga (82), Fredy Haonga (34), Sophia
Mwabenga (18), Ambukusye Kabango (4), Eliud Kibona (3), Anastazia Nzowa (2),
Eliud Msongole (1), Seule Nzowa (1) na Zabron Nzunda (1).
Ileje: Emmanuel Mbuba (98), Gwamaka Mbughi (66) na Emmanuel
Msyani (37).
Tunduma: Frank Mwajoka (130), Victor Nkonjela (20) na
Clemence Nyondo (15).
Momba: David Silinde hakuwa na mpinzani.
Babati Vijijini: Daniel Karenga (14), Esther Sarwatt (17),
Herman Sanka (5), Leonard Mao (3), Salum Shawishi (8) na Lawrence Tara (288).
Arumeru Mashariki: Joshua Nassari amepita bila kupingwa.
Makambako: Olaph Mhema (72), Fred Kalonga (57) na Kheri
Kisingile (0).
Kibaha Mjini: Michael Mtali (62), Henry Msokwa (38), Ishaka
Mnembwe (31), Joachim Mahega (13), Bosco Mfundo (4) na Frank Mzoho (3).
Mbeya Mjini: Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ (356) Christopher
Nyenyembe (12), Joyce Mashine (43), Lazaro Mwankemwa 15, Tito Mwanjale (18) na
Sishe Simbeye (6).
Mbarali: Liberatus Mwang’ombe (110), Jidawaya Kazamoyo
(109), Tazan Ndingo (25), Grace Mboka (14) na Dickson Baragasi (9).
Imeandikwa na Raymond Kaminyoge, Julieth Ngarabali, Shaaban
Lupimo, Faustine Fabian, Stephano Simbeye na Godfrey Kahango na Brand Nelson.
No comments:
Post a Comment