Ligi Kuu soka Tanzania bara kwa miaka kadhaa nyuma kabla ya kuzaliwa kwa klabu ya Azam FC ilikuwa ni ligi ambayo ina ushindani wa kweli kwa timu mbili pekee Simba na Yanga ndizo zilizokuwa na uwezo wa kutwaa taji la Ligi Kuu kwa kupokezana kama sio timu moja wapo kutwaa mara mbili mfululizo.
Hali hii haikutokana kwa sababu ya
ukubwa wa vilabu, hali hii haikutokana kwa sababu ya kuwa na mashabiki
wengi ila ukweli ni vilabu vingi vilikuwa vikikumbwa na tatizo la
kifedha mfano msimu mmoja nyuma tuliwahi kusikia maisha na mazingira
mabovu waliokuwa wanaishi wachezaji wa Stand United kitu ambacho kingeweza kuwa kigumu kuleta ushindani kwa Yanga, Simba na Azam FC.
Baada ya kampuni ya ACACIA inayojishughulisha na masuala ya uchimbaji wa madini kuidhamini klabu ya Stand United, yameanza kutokea mabadiliko chanya
kiasi kwamba msimu ujao inawezekana Stand United ikafanya vizuri. Baada ya kumleta kocha wa kifaransa Patrick Liewig kuinoa klabu yao, July 30 imeonyesha aina ya jezi za kisasa itakazotumia msimu ujao.
ACACIA ni kampuni inayomiliki migodi mitatu ya uchimbaji dhahabu Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara, imeingia mkataba wa udhamini na Stand United katika kipindi cha miaka miwili.
Story na Shaffih Dauda
No comments:
Post a Comment