Uchaguzi mkuu wa Tanzania wa Rais, Wabunge na Madiwani
unatarajia kufanyika Oktoba mwaka huu na tayari watu wenye nia ya kugombea
wameanza kuwashawishi wanachama wa vyama vyao.
Tofauti na miaka mingine, mwaka huu watu wa aina mbalimbali
wamejitokeza wakiwemo waandishi wa habari, wasanii tena vijana kabisa.
Mkuu wa Idara ya habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro
‘Wakimataifa’ amejitoka kusaka nafasi ya kugombea Ubunge katika jimbo la Kawe,
Dar es salaam kupitia Chama Cha Mapinduzi.
Muro na watangaza nia wenzake wanamwaga sera kwa wanachama
wa CCM ili kuteuliwa kugombea.
Swali linabaki pale pale. Jerry Muro atakatwa au hatakatwa
na Wanachama wa CCM?..Tusubiri dakika 90 za siasa….
No comments:
Post a Comment