Jaji Mkuu wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) Roy Sarungi akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo Katika ofisi za Proin Promotions Ltd juu ya mchakato mzima wa fainali ya TMT itakayofanyika tarehe 22 August 2015 Katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Posta kwa kiingilio cha Shilingi Elfu Hamsini (50000) kwa viti maalumu na shilingi elfu thelathini (30000) kwa viti vya Kawaida.Mshindi katika fainali hiyo itaondoka na kitita cha Shilingi milioni hamsini (50,000,000) za Kitanzania.
Meneja Mradi wa Tanzania Movie Talents (TMT) Saul Mpock akiongea kuhusu jinsi Fainali hiyo itakavyorushwa ,moja kwa moja (live) kupitia Kituo Cha Runinga cha ITV pamoja na mitandao mbalimbali ya kijamii , Vilevile amewashukuru wadau wote ambao wameweza kuipiga tafu TMT kwa mwaka huu na kuhaidi kuendelea kukushirikiana nao kwa njia moja au nyingine.
Meneja Bidhaa wa Paisha Godfrey Fataki ambao ndio wadhamini wakuu wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2015 akiongelea juu ya wao kushawishika kuamua kuidhamini Paisha mara baada ya kuona kuna umuhimu mkubwa wa kuinua sekta ya filamu nchini huku akisisitiza Wananchi kutumia app ya paisha katika Simu zao kwaajili ya kuweza Kujipatia bidhaa mbalimbali kutoka kwenye makampuni mbalimbali ambayo yanapatikana ndani ya app hiyo ya Paisha.
Fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2015 itafanyika mnamo tarehe 22 August 2015 katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa kuanzia saa moja na nusu usiku huku fainali hiyo ikirushwa live kupitia kituo cha ITV pamoja na mitandao mbalimbali ya kijamii kama vile blogs.
Fainali hii itakuwa ya kipekee na ya aina yake kutokana na burudani zitakazokuwepo na kuwafanya watazamaji kuendelea kuvutiwa kuangalia shindano hilo mpaka mshindi atakapopatikana na kuibuka na Milioni 50 za Kitanzania huku washiriki wa kumi waliofanikiwa kuingia hatua ya kumi bora wataweza kutengeneza filamu ya pamoja huku wakinufaika na filamu hiyo kuanzia kutengeneza hadi kuuzwa.
Tiketi za fainali zinapatikana Makumbusho ya Taifa Posta, Kwenye Maduka yote ya Hussein Pamba Kali, Dar Live Mbagala, Shear Illusion Mlimani City na Millenium Tower na Tausi Fashion Mlimani City
Shindano la TMT limedhaminiwa na Paisha huku wakisaidiwa na Pepsi, Camgas, Precision Air, ITV/Radio, Global Publishers, I-View Studio, Hartman Barbershop, Van Maria Boutique, Hussein Pamba kali, Data Vision International
No comments:
Post a Comment