Baada ya miaka 31 kupita, Athletic Bilbao wametwaa kombe la kwanza baada ya kuinyuka Barcelona kwa ushindi wa jumla wa magoli 5-1 katika mechi mbili za fainali ya Spanish Super Cup.
Jana usiku, Barcelona wamelazimishwa sare ya 1-1 katika mchezo wa marudiano wa kombe hilo uliopigwa dimba la Camp Nou, wakati katika mechi ya kwanza walikula kichapo cha 4-0.
Lionel Messi aliwafungia Barca goli la kuongoza dakika ya 43' na kufufua matumaini ya kupindua matokeo ya awali, lakini yule yule aliyepiga ha-trick kwenye mechi iliyopita, Aritz Aduriz alifuta baadaye dakika ya 74.
Bahati mbaya zaidi, Gerard Pique alitolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 56, lakini dakika ya 86 Kike Sola wa Bilbao naye alionyeshwa kadi nyekundu.
Hata hivyo Barca wameupiga mpira mwingi, kwani mpaka dakika 90 zinamalizika walikuwa wanaongoza kumiliki mpira kwa asilimia 73 dhidi ya 27 za Bilbao.
Msimu uliopita Barcelona walishinda makombe matatu yaani Treble.
Walitwaa taji la La Liga, Uefa Champions League na kombe la Mfalme.
Kufungwa na Bilbao kunamaanisha wamepoteza kombe la kwanza msimu huu mpya.

No comments:
Post a Comment