Jina
la Jerry Muro sio geni masikioni mwa walio wengi kwani aliwahi kufanya
kazi ya uandishi wa habari za uchunguzi kwa muda mrefu na zilizofanya
jina lake kukua na watu kumtambua, Jerry ambaye kwa sasa ni mkuu wa
idara ya habari ya klabu ya Dar Es Salaam Young African.
Mwaka 2015 aliamua
kuingia rasmi katika siasa kwa kuanza harakati za kutaka kulirudisha
jimbo la Kawe kwa chama tawala, Jerry alikuwa ni miongoni mwa makada 21
wa CCM waliojitokeza kuomba ridhaa ya kugombea ubunge wa jimbo la Kawe
kupitia kwa chama cha mapinduzi (CCM).
Kwa bahati mbaya kura
hazikutosha kumuwezesha Jerry Muro kupata ridhaa hiyo ya kupata nafasi
ya kugombea ubunge wa Kawe kupitia chama cha mapinduzi, ila ameeleza
sababu za yeye kukosa nafasi hiyo na nini kilipelekea yeye kushindwa
katika kura za maoni, hii ni exclusive interview aliofanya na
millardayo.com Jerry Muro ana haya.
“Kweli
nilikuwa mgombea wa jimbo la Kawe kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi
CCM nilikuwa miongoni mwa wagombea 21, tukiwa katika mchakato nilipata
changamoto mbili ya kufiwa na baba yangu na kuvunjiwa nazi na mayai
lakini kubwa ni kufiwa na baba yangu mzee Muro alifariki tarehe 31
wakati sisi tunaelekea ukingoni wa kuitimisha kampeni na alivyofariki
mzee wangu nilisitisha kila kitu”
Hadi sasa Halima Mdee wa
chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA ndiye mbunge rasmi wa jimbo
hilo hadi pale Oktoba 25 uchaguzi mkuu utakapofanyika wa kuchagua
wabunge, madiwani na Rais, Halima Mdee alishinda katika uchaguzi mkuu
mwaka 2010 na kufanya awe mbunge wa jimbo hilo.
No comments:
Post a Comment