Na Mwandishi Wetu
TAMASHA la
manunuzi maarufu kama Pop Up Bongo, ambalo limeandaliwa na kampuni ya Studiored
PR linatarajiwa kufanyika Jumamosi (Agosti 29) katika baa ya Triniti iliyopo
Oysterbay jijini Dar es Salaam kuanzia saa 8 mchana hadi 2 usiku.
Tamasha hilo
linalodhaminiwa na kampuni ya Smirnoff, ni la kwanza na la aina yake kufanyika
jijini ambapo linafungua duka la muda mfupi la manunuzi ya rejareja ambapo
wanunuaji watapata fursa kwa siku moja tu katika eneo maalum.
Maduka ya
Pop Up duniani kote yanafanya mauzo ya rejareja kwa kuwapa wateja uzoefu wa
manunuzi mbadala na wa ubunifu ambao ni tofauti kwa maduka ya rejareja
yaliyozoeleka.
Aidha, bidhaa
zitakazouzwa zitaleta shamrashamra nyingi, ufahamu na kuwapa wateja msisimko
wenye furaha na wa kipekee kufanya manunuzi. Tamasha hilo linafanyika kila baada ya miezi mitatu hadi
minne katika maeneo mbalimbali huku bidhaa mpya zikiuzwa katika kila tukio.
Hii ni fursa
kwa ajili ya wajasiriamali wa ndani kuweza kutangaza bidhaa zao na kuweza kujulikana huku sekta ya fasheni na
mtindo wa maisha ikizidi kukua.
Kampuni
zenye bidhaa zitakazokuwa kwenye tukio hilo ni pamoja na; Secret Habits,
Enjipai, PSJ Couture, Dress Kitenge, Africology, Kaya African Collection, OGS
Studio, Nuya’s Essence, Henna Hub, FT Boutique na Branoz Collections, Happy
Socks, Kipilipili pamoja na DJ Vasley, ambaye atampa kila mtu burdani huku
wakifanya manunuzi kwa siku nzima.
Onesho la
Pop Up Bongo lilizinduliwa Juni 28, 2014 katika eneo la Terrace Slipway, ambako
tukio lililopewa jina la "Lipstick & Lace" likishirikisha wauzaji
wawili wa rejareja- Secret Habits na Atsoko.
Ni tukio
ambalo lilipata mahudhurio mazuri, ambapo wateja 70 hadi 80 waliitumia alasiri
ile kwa kufanya manunuzi na kuburudishwa na muziki pamoja na tafrija na
vinywaji. Tukio la Pop Up Bongo kwa sasa lina wahudhuriaji zaidi ya 400 na
kampuni za bidhaa 15.
Majira haya
ya joto, tunakuletea tukio la 5 la Manunuzi la Pop Up Tanzania na bidhaa zako
uzipendazo. Kipya katika kipindi hiki ni ni "Huduma Maridhawa",
ambapo wageni wanaweza kupata vinywaji ambavyo vitabuniwa na kutolewa bure
baada ya kununua chupa ya Smirnoff.
Pia kipya ni
nembo ya biashara ya Pop Up Polaroid ambayo itawapa wageni fursa kupata
machapisho ya Polaroid ambayo wanaweza kutumiana katika akaunti zao za mitandao
ya kijamii na kuweka kama kumbukumbu ya tukio hilo
"Hii ni
jukwaa la kuuza bidhaa yako kuvuma kipeke nchini Tanzania. Tunataka kuwasaidia
wajasiriamali wa ndani katika sekta kukua, kupata wateja wapya na pia pesa
"anasema Natasha Stambuli, muasisi mwenza wa Pop Up Bongo.
Duka la siku
moja la Pop Up linaunda jukwaa kwa ajili
ya fasheni mbalimbali na mitindo ya maisha ya kampuni za bidhaa mbalimbali
kuweza kuonesha bidhaa zao na kushirikiana na wateja huku wakifurahia alasiri
ya kusisimua wakifanya manunuzi, kucheza muziki na kupata vinywaji.
Natasha
Stambuli, muasisimwenza wa Kampuni ya Pop Up Bongo na mmiliki wa moja ya
kampuni za kijasirianali zinazoshiriki, Tabia Siri, ana shauku ya kupenda kazi
za kijamii. Yeye ni mmoja wa wanachama wa Chama cha Umoja wa Mataifa cha
Tanzania, akifanyakazi pamoja nao kukusanya fedha za kununua vitanda kwa ajili
ya wodi za wazazi nchini Tanzania. Kwa sababu hiI, Sh 1,000 ya kila mauzo
itachangia kwa ajili hiyo.
Tukio la Pop
Up Bongo linaandaliwa na Studiored PR na limeasisiwa na waanzilishiwenza
wengine, Tanya Mulamula na Natasha Stambuli.
Mwisho
No comments:
Post a Comment