
Ofisi
ya Madini, Kanda ya Mashariki Dar es Salaam inautangazia Umma kwamba, usiku wa
Jumapili ya kuamkia tarehe 03-08-2015 wezi walivunja Ofisi ya Madini Kanda ya
Mashariki iliyopo Upanga, Dar es Salaam na kuiba vitu mbalimbali vya Ofisi vikiwemo
vitabu vya Stakabadhi za malipo ya Serikali.
Katika tukio hilo,
stakabadhi namba ERV 6361601-6361800,
na ERV 6361201, 6361202, 6361203, 6361204
ziliibwa.
Kwa taarifa hii, tunautangazia
Umma kwamba stakabadhi zote zilizoibwa na kuharibiwa hazitumiki na malipo yote
yatakayofanyika kupitia stakabadhi tajwa hapo juu yatakuwa ni batili.
Tunaomba yeyote
mwenye taarifa sahihi zitakazoweza kusaidia kukamatwa kwa wezi husika kutoa
taarifa katika Ofisi ya Madini au kituo chochote cha Polisi kilichopo karibu.
Imetolewa na:
Kamishna
Msaidizi wa Madini
Kanda
ya Mashariki – Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment