Kundi
la watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo wamevamia na kuibomoa nyumba
ya mgombea ubunge wa chama cha wananchi CUF jimbo jipya la nanyamba
wilaya ya mtwara vijijini, twahiri saidi baada ya kushindwa kurudisha
fomu ya ubunge na kutokomea kusiko julikana huku simu zake za mkononi
zikiwa hazipatikani.
Wakizungumza
kwa masikitiko baadhi ya viongozi wa chama hicho na wanachi wa jimbo la
Nanyamba wamesema mazingira aliyotoweka mgombea huyo yanaonyesha wazi
kuna mchezo mchafu umefanywa ili kutoa fursa kwa mgombea wa CCM
Abdallah Chikota kupita bila kupingwa katika jimbo hilo.
Akizungumzia
tukio hilo katibu kata wa CUF kata ya Milango Minne eneo analotoka
mgombea huyo, amesema mwisho wa kuwasiliana na mgombea huyo ilikuwa
majira ya saa saba akimuhimiza kuwahisha fomu kwa msimamizi wa uchaguzi.
Hata
hivyo anasema majibu ya mgombea huyo yalionyesha wazi kuna jambo baada
ya kudai hawezi kuacha ajira yake na kuingia kwenye kinyang’anyiri cha
uchaguzi wakati viongozi wa CUF taifa walimuaidi kumpa shilingi milioni
30 kwa ajili ya uchaguzi na wameshindwa kufanya hivyo na baada ya maneno
hayo simu zake hazikuweza kupatikana mpaka muda huu.
Kwa
upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya maji wa nanyamba oscar ng’itu
ambaye aliongozana na mkuu wa kituo cha polisi nanyamba alitembelea
nyumba iliyobomolewa na kutoa agizo kwa wananchi kuwataja watu
waliyohusika na tukio hilo vinginevyo mkono wa sheria utachukua mkondo
wake.
No comments:
Post a Comment