Haiba ya Mnara wa Kumbukumbu ya Miaka Hamsini ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964 inavyoonekana baada ya kumalizika kujengwa hapo katika Majumba ya Maendeleo Michenzani Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein akikata utepe kuashirika kuufungua Rasmi Mnara wa Kumbu kumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964 hapo Michenzani Mjini Zanzibar.
Mshauri wa Ujenzi wa Mnara wa wa Kumbu kumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar Mhandisi Abdul Aziz akimpatia maelezo Rais wa Zanzibar Dr. Shein wakati akiukagua Mnara huo baada ya kuuzindua rasmi.
Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein akiangalia mandhari ya Mji wa Zanzibar katika chombo maalum { Darubini } wakati alipotembelea sehemu mbali mbali za Mnara wa Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar Michenzani baada ya Kuuzindua rasmi.
Mandhari ya Bustani ya Michenzani iliyomo ndani ya eneo la Mnara linavyoonekana kwa juu ya Mnara wa Kumbu kumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Picha na –OMPR – ZNZ.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein amewatahadharisha watu wanaoogopa mabadiliko ya Maendeleo kwamba waachane na tabia hiyo vyenginevyo Dunia bila ya shaka na ajizi itawabadilisha.
Alisema Wazanzibari wanapaswa kwenda na wakati katika kuendesha pamoja na kusimamia masuala yao ili waende sambamba na wananchi wa visiwa vyengine Duniani wanaoonekana kupiga hatua za haraka za Maendelei ya Kiuchuni na Ustawi wa Jamii.
Dr. Ali Mohammed Shein alieleza hayo wakati akizungumza na Watu wa rika mbali mbali ambao wengi wao ni vjana na Watoto mara baada ya kuuzindua Mnara wa Miaka 50 ya Mapinduzi Matukjufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964 uliojengwa katika Majumbe ya Maendeleo Michenzaji Kati Kati ya Mji wa Zanzibar.
Alisema wapo watu wakiwemo baadhi ya watendaji wa Taasisi za Umma wenye madaraka ya kutoa maamuzi ambao wana tabia ya kuogopa Mabadiliko kwa kuchelewesha kuidhinisha miradi ya Kiuchumi inayokusudiwa kuwanzishwa na wawekezaji walioamua kuwekeza hapa Zanzibar.
Rais wa Zanzibar alikemea kwamba tabia hiyo mbaya isiyo na sababu za kimsingi imekuwa ikichelewesha na kuviza Maendeleo ya Wananchi na kupunguza Mapato ya Taifa kupitia uanzishwaji wa miradi hiyo wakati Serikal tayri imeshaweka milango wazi kwa wawekezaji wa ndani na nje ya Nchi.
Aliupongeza Uongozi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar chini ya usimamizi wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko huo kwa juhudi iliyochukuwa ya kujenga mnara huo wenye urefu wa Mita 33.5 ambao utatoa fursda kwa wananchi na wageni kuona mamdhari nzuri ya Mji wa Zanzibar sambamba na kupata huduma za msingi.
Alisema chimbuko la Mnara huo lililoibuliwa na Baraza la Mapinduzi Zanzibar wakati wa maadhimisho ya sherehe za Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar lilikuwa na lengo la kuonyesha vugu vugu la Maendelei ya Zanzibar tokea kufanyika kwa Mapinduzi ya Zanzibar ya Tarehe 12 Januari Mwaka 1964.
Mapema Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar {ZSSF } Nd. Abdulwakil Haji Hafidh alisema ujenzi wa Mnara huo mbali ya kutoa fursa kwa wananachi na wageni kuangalia mamdhari ya Mji wa Zanzibar lakini pia utatoa nafasi kwa wazazi kupata mapumziko huku wakiwasubiri watoto wao wanaowapeleka katika Viwanja vya Kufurahishia Watoto Kariakoo.
Alisema tahadhari hiyo imechukuliwa maalum kwa kuzingatia kwamba Mji wa Zanzibar bado haujawa na maeneo mengi ya kupumzikia kiasi cha kuongezwa maeneo hayo ili kukidhi mahitaji kwa siku zinazotokea kuwa na idadi kubwa ya watu hasa siku za siku kuu ambazo watu wengi huamua kutembelea viwanja hivyo.
Mkurugenzi huyo wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar { ZSSF } alifahamisha kwamba mnara huo utakuwa na sehemu maalum zitakazowekwa kwa ajili ya watu na wageni kujifunza Historia ya Mapinduzi ya Zanzibar, sehemu za kujifunza wachezaji wa michezo mbali mbali maarufu duniani, kuangalia mandhari ya Mji wa Zanzibar pamoja na Mkahawa unaozunguuka.
Alisema taasisi za Fedha kama Benki ya Wananachi wa Zanzibar PBZ, na Ile na NMB zitatoa huduma za fedha kwa kutumia mtandao wa ATM ili kuwaondoshea usumbufu wateja wao wakati wanapoishiwa na Matumizi.
Nd. Abdulwakili alieleza kwamba katika kulibadilisha eneo hilo la Michenzaji Mfuko huo umeshaandaa mpango wa kujenga majengo la Kimataifa ya Kibiashara { SHOOPING MALLS } upande wa Kaskazini kwa kutafuta washikika wa Maendeleo watakaoshirikiana katika kujenga majengo hayo.
Mnara huo wa Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar wenye ghorofa 9 uliojengwa kwa gharama ya Shilingi za Kitanzania Bilioni Nane unatarajiwa kurejesha thamani ya Fedha hizo katika kipindi cha miaka 12 ijayo.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
No comments:
Post a Comment