Pichani ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Hali halisi Saed Kubenea akiyatambulisha matoleo ya Magazeti mwanahalisi yaliyosababisha Gazeti kufungiwa picha na Maktaba |
HATIMAYE
Mahakama kuu imelifungua rasmi Gazeti la Mwanahalisi ambalo lilifungiwa
na serikali kwa mda usiojulikana .Anaandika KAROLI VINSENT endelea
nayo.
Akizungumza Mhariri wa Gazeti la Mwanahalisi
,Jabir Idrisa amethitisha kuwa Jaji wa mahakama kuu Salvatory
Bongole,amelifungulia Gazeti hilo na kulitaka liendelee na kazi yake ya
kuhabarisha umma baada kubainika katika kulifungia kwake kanuni
zilikiukwa.
Amesema hukumu hiyo imetokana na kesi namba 27 ya mwaka 2013 ambapo
Kampuni ya Hali halisi limited ambao ni wachapishaji wa Gazeti la
Mwanahalisi walikuwa wakitaka patio la hatua ya waziri wa Habari Fenera
Mukangala juu ya kulifungia Gazeti hilo, Katika kesi ambayo
iliwakilisha kwa Upande wa
Serikali na ofisi ya Mwanahseria mkuu wa Serikali
Serikali na ofisi ya Mwanahseria mkuu wa Serikali
Jabir
amesema Mahakama imebaini waziri wa Habari hakufuata sheria katika
kulifungia gazeti hilo,licha ya kuwa na mamlaka ya kutokana na sheria ya
Kandamizi ya Magazeti ya mwaka 1976 inampa uwezo wa kulifungia
gazeti,
Amesema Sheria iyo inamtaka waziri husika kufuata hatua kabla ya
kulifungia Gazeti ambapo hatua hiyo ni kuwafuata wale anawaowatuhumu ili
wapate utetezi na kuchukua hatua lakini waziri huyo alipolifungia
Gazeti hilo hakufuata hatua hizo.
HATUA GANI INAFUATA BAADA YA HUKUMU HIYO.
Mwandishi
huyo mwandamizi amesema kwa sasa kinachofuata ni kutaka fidia toka
serikalini juu ya hasara iliyopatika wakati Gazeti hilo lilipokuwa
limefungiwa huku akisema mahakama imeamulu wafanye hivyo.
Amesema Chengine kinachofuata ni mwenyewe Mmiliki wa Gazeti hilo
akiamua kuchapisha Gazeti hilo anachapisha au aache kutokana na
mahakama hiyo kumruhusu.
Kufunguliwa huko kwa Gazeti la kiuchunguzi la Mwanahalisi kunakuwa ni kama ushindi kwa Mkurugenzi wa Gazeti Saed Kubenea Mara kwa mara amekuwa ikidai serikali kulifungulia Gazeti hilo kimakosa……
No comments:
Post a Comment