Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, September 11, 2015

KASORO KATIKA KIZAZI ( UTERINE SEPTUM)

Hii ni hali ambayo mwanamke anazaliwa akiwa na kasoro katika kizazi, ni kasoro ya kuzaliwa nayo ambayo mwanamke mwenyewe hajui.
Kizazi hugawanyika katikati tokaa juu hadi chini. Kizazi chenye kasoro hizi huonekana cha kawaida kwa nje lakini tatizo lipo kwa ndani. Mgawanyiko huu unaweza kukamilika au usifike mwisho.
Mwanamke mwenye tatizo hili pia huwa na milango miwili ya kizazi ‘Double Cervix’ na hata kasoro ikiwa kubwa huwa na sehemu mbili za uke.
CHANZO CHA TATIZO
Kama tulivyoona, tatizo hili ni la kuzaliwa nalo hivyo basi mwanamke huumbwa hivyo na tatizo huanzia katika kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito ambacho ni kipindi cha uumbaji, kitaalam kinaitwa ‘Embrogenesias’ ambapo sehemu maalum ya kuumba kizazi huungana pamoja.
Sehemu hiyo baada ya kuungana huendelea vizuri na kutengeneza kizazi kamili kisicho na kasoro lakini ikitokea hitilafu katika sehemu hiyo basi haiungi vizuri na kusababisha kasoro hizo.
HALI YA TATIZO KWA UJUMLA
Kwa mujibu wa utafiti tofauti kwa wanawake mbalimbali inaonesha kwamba wanawake wenye tatizo hili husumbuliwa zaidi na tatizo la kuharibikiwa na mimba. Utafiti uliofanywa na mwanasayansi Woelfer na wenzake umeonesha baadhi ya wanawake wenye tatizo hili ambapo wameligawa katika makundi mawili, ‘Arcuate uterus’ na ‘Bicornuate uterus’.
Katika taarifa yao imeonesha takriban wanawake wengi ambao mimba zao huharibika mara kwa mara au hupoteza ujauzito mara kwa mara tatizo kubwa ni kasoro za kizazi kama tulivyoona.


DALILI ZA TATIZO
Mwanamke hawezi kujua kama ana tatizo hili, atakuwa katika hali ya kawaida kama mwanamke lakini kila akipata ujauzito unatoka, ila inaweza kutokea akapata ujauzito kawaida lakini ukawa katika hatari kubwa ya kutoka au kuzaa kabla ya mtoto hajakomaa. Vilevile  mtoto anaweza kukaa vibaya katika mfuko wa uzazi.
Mimba zilizopo katika mfuko wa kizazi wenye kasoro pia zinaweza kuvuka miezi mitatu ya kwanza na kutoka katika miezi mitatu ya pili lakini nyingi hutoka katika kipindi hiki cha miezi mitatu ya kwanza.
UCHUNGUZI
Daktari atamfanyia mgonjwa kipimo kiitwacho ‘Pelvic examination’ ambacho kitaonesha endapo ana sehemu mbili za uke au mlango wa kizazi, lakini pia anaweza kuwa na maumbile ya kawaida ila kasoro zikawa kwa ndani ambazo hazitaonekana katika ‘Pelvic examination’.
Vipimo vingine ni kama daktari atakavyoelekeza, ili kuthibitisha uwepo wa kasoro inatakiwa ushirikiano wa dhati kati ya mgonjwa na daktari wake kwani baadhi ya vipimo huwa na gharama.
MATIBABU NA USHAURI
Tatizo la kasoro ya kizazi likishagundulika hutibiwa kwa upasuaji ambapo ‘partition’ iliyojitengeneza au kuumbwa huondolewa kwa makini.
 Upasuaji huwa mkubwa pia hutegemea na kasoro zilizopo mfano endapo kama uke au mlango wa kizazi pia upo katika sehemu mbili.
Wanawake wenye tatizo hili huishia kuwa wagumba kutokana na kupoteza mimba nyingi, unaweza kupoteza hata mimba tatu au zaidi

No comments:

Post a Comment