Bondia na mwanamichezo tajiri zaidi duniani Floyd ‘money’ Mayweather amemtupia maneno ya kejeli bondia mwenza Manny Pacquiao kwamba inabidi asubiri yeye astaafu ndio atabaki kuwa bondia bora.Floyd ameyasema hayo akiwa MGM Arena kujiandaa na pambano lake la mwisho dhidi ya Andre Beto ambalo litakua la 49 na kwamba hatopigana tena. Floyd akasema pamoja kunamabondia wengi kwenye game ya ngumi, lakini uzoefu utambeba Pacquiao kuwa bora pindi yeye akistaafu.
Kauli hiyo ya Mayweather ni ya kejeli kwa Pacquiao ambaye alimchukia tangu alipotangaza kuwa alipigana na Mayweather akiwa na maumivu ya bega kitu kilichomuudhi Floyd aliyeamini Manny Pacquiao analeta visingizio badala ya kukubali matokeo.
Bondia Floyd Mayweather atapanda ulingoni tarehe 12 mwezi huu kupambana na Mmarekani mwenza Andre Berto katika pambano lake la mwisho la career yake ya ngumi na kama akishinda basi atakua ameweka rekodi ya aina yake ya kutopoteza hata mchezo mmoja kwani hadi sasa ameshinda michezo yote 48 aliyocheza.
No comments:
Post a Comment