Mh.Paul Makonda akizindua vitabu
Mkuu
wa Wilaya Kinondoni Mh.Paul Makonda siku ya jana katika kanisa la
Living Water Center chini ya mtumishi wa Mungu Apostle Onesmo Ndegi
alikuwa mgeni wa heshima katika uzinduzi wa vitabu vitatu "MJUE MWANAMKE,USIIPE HOFU NAFASI na RAFIKI ANAYEKUFAA vilivyoandikwa na Mwl Lilian Ndegi wa Kanisa la Living Water Center Kawe.
Ibada
hiyo ya uzinduzi wa vitabu ilipambwa na vikundi vya uimbaji sifa kama
Living Waters wenyeji Upendo Nkone,GUG Dancers na More Than Enough Band.
Mkuu
huyo wa wilaya ndiye aliyezindua vitabu hivyo na kuendesha zoezi zima
la uuzaji wa vitabu hvyo,kwa kuanza alinunua vitabu hivyo vitatu kwa
shiling Milioni 5 ikiwa ni kuchangia na kusapoti huduma hiyo ya uandishi
wa vitabu vya Mwl Lilian Ndegi ambaye ni Mama yake kwa malezi ya kiroho
kanisani hapo Living Water Center Kawe.
Katika
uzinduzi huo uliambatana na kukata keki ikiwa ni ishara ya kufurahia
mafanikio ya kazi ya uandishi wa Mwl Lilian Ndegi na ugawaji wa zawadi
katika tukio hilo ulifanyika kwa watu ambao wamekuwa wakihusika katika
ufanikishaji kwa namna moja au nyingine au kumuwezesha Mwl Lilian
kufanikisha uandishi wake wa vitabu.
Mh
Paul Makonda aliwasihi washirika wa Kanisa la Living Water Center Kawe
kusapoti kazi ya Mwl Lilian ikiwa ni kwa kununua na kuvisambaza vitabu
vyake ili viwafikie wasomaji wengi ikiwa vitaleta matokeo mazuri katika
maisha yao kutokana na ujumbe ulio ndani ya vitabu hivyo.
Apostle
Onesmo Ndegi kiongozi wa Kanisa la Living Water Center na mme wa
mwandishi wa vitabu Mwl Lilian Ndegi katika kuzungumza kwake alikuwa
akijivunia Mkuu huyo wa Wilaya na kusema ni kijana wake anamfahamu
vizuri siku nyingi tangu bado anasoma na kusema amelelewa hapo na kusema
kuwa alikuwa msikivu,na mpaka Mh Rais kumteua kwa nafasi hiyo ya kuwa
Kiongozi wa Wilaya hakukosea.
|
No comments:
Post a Comment