Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na
bia ya Kilimanjaro, Charles Mkwasa (pichani) amesema kikosi chake kipo tayari
kwa mchezo wa kesho dhidi ya Nigeria kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya
Afrika mwaka 2017.
Akiongea na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa mikutano wa
TFF uliopo Karume, Mkwasa amesema vijana wake wapo katika hali nzuri kuelekea
kwenye mchezo huo wa kesho ambao ni muhimu kwa Taifa Stars.
“Tumefanya mazoezi kwa takribani siku kumi, vijana wako katika hali
nzuri ya mchezo, uwezo waanaouonyesha mazoezini ni wa hali ya juu na unatupa
matumaini ya kufanya vizuri” Alisema Mkwasa.
Aidha Mkwasa amesema katika mpira hakuna kinachoshindakana,
anatambua Nigeria ni timu kubwa Afrika, wameshatwaa ubingwa wa Afrika mara
tatu, lakini mpira wa sasa lolote linaweza kutokea, hivyo sisi tumejiandaa
vilivyo kufanya vizuri katika mchezo huo.
Mwisho Mkwasa amesema wamejindaa vizuri kwa mchezo huo wa kesho, na
kuwaomba watanzania kuja kuwapa sapoti wachezaji uwanjani kwa kuwashangilia
muda wote wa mchezo, na kusema kikosi chake hakina mchezaji majeruhi hata mmoja
kuelekea kwa mechi hiyo.
Mechi hiyo ya kesho jumamosi itachezeshwa na waamuzi kutoka nchini
Rwanda ambao ni Louis Hakizimana (mwamuzi wa kati) Honore Simba (mwamuzi
msaidizi), Jean Bosco Niyitegeka (mwamuzi msaidizi), Abdoul Karim Twagiramukiza
(mwamuzi wa akiba) na kamisaaa wa mchezo ni Charles Kasembe kutoka nchini
Uganda ambao wote tayari wameshawaili jijini Dar es salaam tangu jana jioni.
No comments:
Post a Comment