Pages

Saturday, September 5, 2015

SUPERSPORT KWENDA LAIVU ALL AFRICAN GAMES

D3A_3549
Meneja Mkuu wa SuperSport kwa ukanda wa Kusini mwa Afrika, Graeme Murray akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kutoka nchi za Afrika (hawapo pichani) katika hoteli ya OutriggerHotel & Beach Resort nchini Mauritius.
Na Modewjiblog, Mauritius
WAKATI leo michezo ya 11 ya All African games chaneli ya SuperSport imetangaza rasmi kwamba watashika usukuni wa kurusha matangazo ya michezo hiyo kupitia SuperSport 9 Michezo hiyo imeanza juzi.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa uzalishaji wa SuperSport, Alvin Naicker wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mkusanyiko mkubwa wa MultiChoice uliohusisha waandishi wa habari, masupastaa na chaneli wanazofanya kazi nazo katika hoteli ya OutriggerHotel & Beach Resort nchini Mauritius.
Akiwa mtu kati Naicker alisema kwa kujiamini kwamba urushaji wa matangazo hayo ni sehemu ya uuzaji wa sura ya michezo ya Afrika katika mabara mengine.
Akiwa katika mazungumzo hayo ambayo yalioongozwa na mmoja wa watu wanaotoa burudani kubwa ya utangazaji ndani ya SuperSport, Carol Tshabalala alisema hali hiyo inatokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa katika sekta nzima ya burudani na michezo na kampuni ya MultiChoice.
D3A_3571
Mkuu wa masoko wa SuperSuport, Motheo Matsau akifurahia jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika visiwa vya Mauritius.
Katika mazungumzo hayo ambapo pia alikuwapo Mkuu wa masoko wa SuperSuport, Motheo Matsau, Meneja mkuu wa SuperSport kwa ukanda wa Kusini mwa Afrika, Graeme Murray na mgeni maalum Anthony Baffoe, mchezaji wa zamani wa kimataifa na Mratibu mkuu wa FIFA na CAF, Naicker alisema ubora wa chaneli yake unatokana na kuweza kunoa vipaji vya watangazaji wake kufikia kiwango cha juu kabisa cha ubora.

Kama mwekezaji mkubwa wa masuala ya michezo katika bara la Afrika, SuperSport imepata matokeo ya kuridhisha na yenye tija.
“Mwaka 2006 tulipeleka kundi dogo la watu 26 Abudja kutangaza mpira lakini leo hii tunaringia kuwa na asilimia 100 ya watangazaji wenyeji wakifanyakazi zao katika nchi za Nigeria na Ghana,”alisema Murray.
Baffoe naye aliongeza kwamba mchango wa SuperSport umeongeza zaidi ya utangazaji na kuwezesha kuongezeka kwa kiwango cha uprofesheni katika ligi mbalimbali barani Afrika.
D3A_3677
Mchezaji wa zamani wa kimataifa na Mratibu mkuu wa FIFA na CAF, Anthony Baffoe akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani).
“SuperSport iliweka msingi wa utoaji leseni kwa klabu, kuwaelimisha watawala, kuweka viwango vya msingi katika viwanja, kusaidia kuanzishwa kwa umoja wa wachezaji, kuwafanya wachezaji kuwa wadau muhimu katika ligi na kuwaruhusu wajipange kwa maisha nje ya soka,” alisema.
Murray alielezea jinsi watangazaji walivyoweza kujishirikisha katika ligi za wenyeji kama mfano bora namna ambavyo Supersport imesaidia michezo katika bara hili
“Tulianza kushirikiana na Ligi Kuu ya Nigeria mwaka 2006 na imeendelea kukua mwaka hadi mwaka,” alisema. “Tuliweza kuingia katika Super Eagles’ League ya Nigeria na ligi ya kikapu ya Nigeria, ligi zote mbili zinafanya vyema kuliko hapo awali.Tumekuwa washirika wa Ligi Kuu ya Kenya kuanzia mwaka 2008 na Ligi Kuu ya Ghana toka mwaka 2012. Inatakiwa kukumbukwa kwamba kabla ya kuingia kwetu Kenya hakuna hata mechi moja ya ligi iliweza kutangazwa katika runinga na sasa ligi inazidi kukua.”
D3A_3659
Mkuu wa uzalishaji wa SuperSport, Alvin Naicker akisisitiza jambo katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani).
Aidha SuperSport katika siku za karibuni imekamilisha mkataba na waendeshaji wa Ligii kuu ya Zambia kuendelea kuonekanakana katika Supersport kwa miaka mitano ijayo.
Aidha chaneli ya SuperSport inajipanga kuanzisha jarida nchini Zambia litakalouza soko la Zambia kwa mataifa ya Afrika.
Mkuu wa masoko wa SuperSport, Motheo Matsau pia ameongeza kwamba kunahitajika kuuza kwa michezo bara la Afrika na kwa yakini kama maendeleo yaliyopo hayataonekana kwa dunia , itakuwa hakuna maana, kinachojalisha ni kwa kadamnasi ya kimataifa kujua kwamba Afrika ina vipaji bora kabisa katika michezo.
Alisema kupitia matangazo ya chaneli hiyo kunaonesha kwamba mauzo yanaleta faida kama ulivyo mchezo wenyewe na hilo ndilo linafanya Super Sport kuwa chaneli bora zaidi duniani.
Wakati mtu akitoka katika mafunzo ya utangazaji ya chaneli hii anajua michezo na ajui namna ambavyo masuala ya utangazaji yanavyofanyakazi. Watu hawa wanakuwa mabalozi wetu na vyanzo muhimu sana vya habari.Tunatia SuperSport uhai kwa kuwakutanisha watu hawa.”
Naicker katika mazungumzo hayo alisisitiza kuendelea kuwepo kwa mahusiano mazuri kati ya SuperSport na wadau wa michezo wa bara la Afrika.
“Sisi si kwamba tunalipa fedha kwa ajili ya kupata kibali cha kutangaza au kupiga picha za video tukio la burudani hii, lazima kuwepo na utoaji wa elimu, mchakato unaostahili kukabiliwa na pande zote mbili.
Tunapaswa kujua muda gani unastahili kuchezwa na mambo gani ambayo hayastahili kuyatangaza. Tumetengeneza kijarida cha utangazaji ili kila mmoja aweze kusoma kuwasaidia wengine katika mchakato wa namna matangazo yanavyorushwa na ushawishi wake lojistiki, usahihi wa muda na upangaji fixtures. Tunataka ujenga ushirikiano wenye ufanisi kwa muda mrefu,” alisema.
Naicker pia alitumia nafasi hiyo kuelezea furaha yao ya kupata zabuni ya kutangaza michezo ya olimpiki ya mwaka 2016.
D8A_1013
Carol Tshabalala wa Supersport akiendesha mkutano na waandishi wa habari.
“Tutakuwa chaneli nyingi za michezo hiyo, kiwango cha chini kabisa zikiwa ni chaneli 6 kwenye SuperSport bouquet,” alisema.
“Tutarusha kila tukio ambalo mwafrika ana nafasi ya kutwaa medali. Tumetengeneza makundi ya watangazaji na timu zao kufuatilia timu za Kiafrika katika tukio hilo kubwa. Aidha tayari tumeshaanza mazungumzo na mamlaka kubwa za michezo katika nchi za bara la Arika kujua watu ambao wanaweza kutwaa medali ili kuanza kuandaa stori zao kuelekea michezo ya Olimpiki.”
“Tunajivunai si tu kuwa watangazaji wazuri wa michezo katika bara la Afrika, bali duniani,” anasema Naicker.
Kwa kuwatumia masupastaa wa Afrika kama akina Sammy Kuffour kuelezea masuala ya kiufundi na utaalamu wa ndani unachokiona, kusaidia kunyanyua michezo kutoka katika ngazi za awali chini kabisa kwa kuwa na miradi maalumu, SuperSport inaongoza katika kuelezea mafanikio ya Afrika katika michezo kwa mataifa mengine duniani.
Mwandishi wa habari hizi na wengine kutoka nchi mbalimbali za Afrika wapo nchini Mauritius katika moja ya maonesho makubwa ya watoa burudani kwa njia ya televisheni na video ya MultiChoise wanaotumia mtandao wa DSTV na GoTv.
D3A_3541
Carol Tshabalala wa SuperSport.

No comments:

Post a Comment