Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, September 9, 2015

TASWIRA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KWA WANAWAKE KUPITIA VIPODOZI VYA LUV TOUCH MANJANO

  Mkurugenzi Mtendaji   8020 Fashion na  Mentor wa Taasisi ya Manjano Foundation Shamim Mwasha Akitoa Mada kwenye Semina ya Kuwawezesha  Wanawake Kuwa Wajasiriamali kupitia Vipodoz Vya Luv Touch Manjano Iliyoandaliwa na Manjano Foundation Kwa Lengo la Kuwajengea Udhubutu Wanawake  Kufanya biashara pia namna ya Kujiwekea Akiba na Kutumiza Malengo yao.
Washiriki wa Mafunzo hayo  wakisikiliza kwa Makini Mada Mbalimbali zilizokuwa Zikijadiliwa.
 Mafunzo ya Ujasiriamali kwa Mwanamke wa Kitanzania kwa Kutumia Vipodozi vya LuvTouch Manjano yanaendelea.Mradi huo ulianzishwa kuwejengea Uwezo wanawake Kwenye Ujasiriamali yakisimamiwa na Taasisi ya Manjano Foundation.
 
 Lengo la Mradi huo ni kuona kwamba wanwake hawa wanajisimamia na kujikita vizuri kwenye Biashara ya Vipodozi na kujua Mbinu Mbalimbali za Biashara zao kwa lengo la kumuongezea ajira mwanamama na kuondoa dhana za ukosefu wa ajira kuwa chungu ya yeye kujiwezesha katika kujikimu mahitaji yake ya msingi, yaani aweze kujipatia Chakula, Malazi na Mavazi kwa kupitia ujasiriamali.
 Pamoja na mafunzo ya biashara, washiriki hawa watanufaika na utaalamu (Proffessional Makeup Artist).Taasisi ya Manjano Foundation, ambayo imeanzisha jukwaa kwa ajili ya kuandaa miradi na programu ambazo zitamuinua mwanamke wa Kitanzania kwa kumwondolea ugumu wa kipato na ambayo itakuwa ni chachu ya kubadili yale yote yaliyoyazunguka maisha yake. Taasisi hii limekwishazindua mradi wenye kubeba bendera yake, Manjano Dream-Makers, mradi unaokusudia kuzaa kizazi kipya cha wajasiriamali wanawake kwa kutumia kipodozi cha LuvTouch Manjano tu
 Mradi huu Uzinduliwa mwezi Mei mwaka huu na Mama Tunu Pinda. 
Mafunzo haya yametolewa kwa zaidi ya Wanawake 30 ambapo wengi wao tayari wameshaanza kunuafaika na kipodozi pendwa cha LuvTouch Manjano ambapo wamewezeshwa
 
Washiriki hao wakiwa kwenye Picha ya Pamoja

No comments:

Post a Comment