Huu ndio ukweli:-VIJANA wanaomuunga mkono Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, kwa nyakati tofauti jana wamemshangilia kiongozi huyo wa zamani wa CHADEMA, kwenye mkutano wa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA chini ya mwamvuli wa UKAWA, Edward Lowassa.
Hali hiyo ilijitokeza baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe
na Mbunge wa Kigoma Kusini anayegombea tena nafasi hiyo kupitia NCCR
Mageuzi, David Kafulila, kwa nyakati tofauti kumzungumzia Zitto na chama
chake cha ACT-Wazalendo.
Akizungumza kwenye mkutano huo uliofanyika kwenye viwanja vya Mwanga
Community Centre, David Kafulila, aliwataka wakazi wa mkoa wa Kigoma
kumchagua Edward Lowassa na UKAWA, na kwamba nje ya UKAWA vyama vingine
ni miradi ya CCM.
Alisema; “Lowassa ndiye mgombea mwenye sifa za kuwa rais wa nchi hii.
Ndiye pekee toka ameondoka madarakani serikali imesimama kiutendaji.
Huu ni mwaka mbao
tunafanya mafuriko ya kuitoa CCM kwa sababu ni chama ambacho hakikubaliki Kanisani wala Misikitini.”
tunafanya mafuriko ya kuitoa CCM kwa sababu ni chama ambacho hakikubaliki Kanisani wala Misikitini.”
Akiendelea kuzungumza Kafulila alisema kuwa Kigoma haina chama na
kama Kigoma wanataka kuwa na chama kinapaswa kuwa chama cha Mawese
(mafuta yatokanayo na zao la mchikichi) na sio chama cha siasa, na baada
ya kauli hiyo walisikika vijana wakizomea na kupunga mikono ya
kuashiria kutokubaliana nayo huku wakiimba jina la Zitto,video ya tukio hilo nimekuwekea hapo chini mdau wa dutigite.com.
Ikumbukwe kuwa Zitto Kabwe, mara kadhaa aliwahi kutamka kwenye mikutano yake mkoani hapa kuwa ACT-Wazalendo ni chama cha Kigoma.
Nae Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alisema kwenye mkutano huo
kuwa amepata taarifa kwamba katika uchaguzi wa mwak huu Kigoma
kunapepesuka kisiasa baada ya viongozi wawili wa zamani wa CHADEMA,
Zitto Kabwe, anayegombea jimbo la Kigoma Mjini kupitia ACT na Aman Warid
Kabourou anayegombea kupitia CCM.
Kauli hiyo ilifuatiwa na kelele za kuzomea kutoka upande mmoja wa eneo la mkutano huo.
Mbowe aliongeza kuwa Kigoma haina historia ya vyama vya upinzani kupambana na vyama vingine vya upinzani bali kupambana na chama kilichoko madarakani, hivyo kuwataka kuunganisha nguvu kwa kuwa kauli ya wengi ni kauli ya Mungu.
Mbowe aliongeza kuwa Kigoma haina historia ya vyama vya upinzani kupambana na vyama vingine vya upinzani bali kupambana na chama kilichoko madarakani, hivyo kuwataka kuunganisha nguvu kwa kuwa kauli ya wengi ni kauli ya Mungu.
Akizungumza kwenye mkutano huo mgombea urais wa UKAWA, Edward
Lowassa, aliahidi kufanya mageuzi kwenye umeme, maji, kilimo, elimu na
miundombinu ya Reli, na kuwataka wampe kura za uhakika ili aweze
kutimiza ahadi hiyo.
Zitto kupata habari hizi aliandika haya maneno kwenye ukurasa wake wa twitter:-
Asante sana. Watu wa Kigoma, wauza mawese ndio waamuzi ya hatma yetu.
Zitto kupata habari hizi aliandika haya maneno kwenye ukurasa wake wa twitter:-
" watu wa Kigoma wana uwezo wa kuuza mawese tu " - David Kafulila. Tarehe 4 Septemba 2015, Mwanga Centre, Kigoma.
Asante sana. Watu wa Kigoma, wauza mawese ndio waamuzi ya hatma yetu.
...mtandao wa dutigite.com ndio mtandao wa wana Kigoma unaokuletea habari za ukweli na uhakika toka nyumbani Kigoma,unaweza kujiunga nasi moja kwa moja ili tukusogezee kila habari tunayo ipandisha hapa,ingia=>>HAPA
No comments:
Post a Comment