Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu akiwa amepokea kadi kutoka kwa wanachama wa CHADEMA waliojiunga na CCM baada ya kukihama chama hicho. Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu.
Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu.
Baadhi ya vijana wakiwa wamepanda juu ya miti ili kushuhudia mkutano wa kampeni wa Bi. Samia Suluhu. Burudani ya wasanii wa ngoma za asili katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu. Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu. Mgombea ubunge wa Jimbo la Kibakwe akizungumza na wanaCCM katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu. Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu akipokea kadi kutoka kwa wanachama wa CHADEMA waliojiunga na CCM baada ya kukihama chama hicho Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu akipokea kadi kutoka kwa wanachama wa CHADEMA waliojiunga na CCM baada ya kukihama chama hicho.[/caption]
Na Joachim Mushi, Dodoma
MGOMBEA mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu amesema Serikali itakayoundwa na chama hicho endapo itashika dola katika Uchaguzi Okuu wa Oktoba, 2015 itahakikisha inapima ardhi yote ya vijiji pamoja na kuainisha mipaka ili kukomesha migogoro ya ardhi.
Bi. Suluhu ametoa kauli hiyo alipokuwa akinadi ilaya ya CCM katika Majimbo mawili tofauti ya Kongwa na Chilonwa Mkoa wa Dodoma ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake za kufanya kampeni kuwashawishi Watanzania waweze kuipa ridhaa tena Chama Cha Mapinduzi ili kiunde Serikali na kuwatyumikia wananchi.
Mgombea huyo mwenza wa urais akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Chilonwa Kijiji cha Nzali alisema Serikali ya CCM kwa kushirikiana na halmashauri itaipima ardha ya vijiji na kuweka mipata hasa maeneo sugu ya migogoro kama Kongwa na Kiteto ili kuzuia migogoro na mapigano kwa jamii hizo mbili.
Alisema mara baada ya kupima ardhi na kuweka mipaka kati ya maeneo ya wakulima na wafugaji watahakikisha mipaka hiyo inatambulika na kuheshimiwa na jamii zote mbili ili kuzuia migogoro na mapigano ambayo yamekuwa na uhasama mkubwa na kupoteza uhai na mali za raia wasio kuwa na hatia katika maeneo yenye mgogoro.
Ardhi ya Tanzania ni yetu sote haina haja ya kugombana sisi kwa sisi, tutapima ardhi ya vijiji vyote ili mipaka ionekane ikiwa ni pamoja na kuainisha maeneo ya wafugaji, wakulima na pia kumalizia miradi ya maji iliyosimama katika baadhi ya vijiji ili viweze kupata huduma hiyo.
Bi. Suluhu pia aliwapokea wanachama saba (7) wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambao walirudisha kadi za CHADEMA na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi na kukabidhiwa kadi mpya za CCM. Aliwapongeza wananchama hao kwa kugunduwa mapema kuwa wamepotea chama kwa kujiunga na chama kisichokuwa na mwelekeo.
Aidha aliongeza kuwa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi itashughulikia kero ya mawasiliano ya simu katika baadhi ya vijiji katika maeneo hayo ikiwa ni pamoja na kumalizia miundombinu ya barabara tegemezi kwa maeneo husiki ikiwa ni ishara ya kuchochea maendeleo. Awali akizungumza mgombea Ubunge katika Jimbo la Kongwa, Job Ndugai alisema ilani ya Chama Cha Mapinduzi jimboni hapo imetekelezwa kwa asilimia 95, kuanzia miradi ya umeme, maji, elimu na miundombinu hivyo wanaKongwa hawana budi kuichagua CCM.
No comments:
Post a Comment