Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza katika hafla ya kukabidhi madawati 200 kwa Shule ya Msingi Buyuni iliyopo ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam. Madawati hayo yametolewa na Benki ya CRDB ili kukabiliana na upungufu wa madawati shuleni hapo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza katika hafla ya kukabidhi madawati 200 kwa Shule ya Msingi Buyuni iliyopo ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam. Madawati hayo yametolewa na Benki ya CRDB ili kukabiliana na upungufu wa madawati shuleni hapo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (wa pili kushoto) akikata utepe wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa madawati 200 kwa Shule ya Msingi Buyuni iliyopo Chanika katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja wa Benki hiyo tawi la Kariakoo, Andrew Augustine, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Asha Mapunda (wa pili kulia) na Mkuu wa shule hiyo, Maulidi Maliki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk.
Charles Kimei (wa pili kushoto) akikata utepe wakati wa hafla ya kukabidhi
msaada wa madawati 200 kwa Shule ya Msingi Buyuni iliyopo Chanika katika
Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja wa Benki hiyo
tawi la Kariakoo, Andrew Augustine, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya
Ilala, Asha Mapunda (wa pili kulia) na Mkuu wa shule hiyo, Maulidi Maliki.
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Shule Buyuni, Maulidi Maliki, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk.
Charles Kimei, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Asha Mapunda na Meneja wa Benki wa Benki ya CRDB tawi la Kariakoo, Andrew Augustine wakipiga makofi baada ya Benki ya CRDB kukabidhi msaada wa madawati 200
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk.
Charles Kimei akimkabidhi keki ya maalum ya shukrani Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Asha Mapunda wakati wa hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charle Kimei
(kushoto), akikagua sehemu ya madawati 200 yaliyokabidhiwa na Benki ya CRDB kwa uongozi wa Shule ya Msingi Buyuni. Kulia ni Meneja wa Benki hiyo tawi la
Kariakoo, Andrew Augustine.
Wanafunzi wakiwa wamekaa katika madawati waliokabidhiwa na Benki ya CRDB.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Buyuni
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei
(kushoto) akiangalia sehemu ya madawati 200 yaliyokabidhiwa na Benki ya CRDB
kwa uongozi wa Shule ya Msingi Buyuni iliyopo Chanika wilaya ya Ilala jijini
Dar es Salaam. Katikati ni Meneja wa Benki hiyo tawi la Kariakoo, Andrew
Augustine na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Asha Mapunda.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charle Kimei
(Katikati) akiwa na Mkuu wa Shule ya Msingi Buyuni, Maulidi Maliki (wa pili
kushoto), Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Asha Mapunda (kulia) na Meneja wa Benki hiyo tawi la
Kariakoo, Andrew Augustine (wa pili kulia), wakiwa pamoja na wanafunzi wa shule
hiyo baada ya kukabidhi madawati 200 yaliyotolewa na uongozi wa Benki ya CRDB.
Hafla ya makabidhiano ilifanyika Dar es Salaam.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Buyuni wakiwa na furaha baada ya uongozi wa Benki ya CRDB kukabidhi madawati 200.
Sehemu ya madawati yaliyotolewa na Benki ya CRDB.
Madawati 200 yalitolewa na Benki ya CRDB.
Na Mwandishi Wetu
BENKI ya CRDB imetoa msaada wa madawati 200 yenye thamani ya sh
milioni 20 katika Shule ya Msingi Buyuni iliyopo katika Manispaa ya Ilala, Dar es Salaa
ikiwa ni mwendelezo wa wiki ya huduma kwa wateja wake.
Akikabidhi madawati hayo shuleni hapo Mkurugenzi Mtendaji
wa CRDB, Dk. Charles Kimei alisema huo ni mchango wa benki hiyo kwenye sekta ya
elimu inayoithamini.
Mbele ya wazazi, Kamati ya shule, walimu na mwakilishi wa
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Dk. Kimei alisema benki yake imechangia pato
la taifa kwa kulipa kodi ya sh bilioni 50 kwa serikali huku akisisitiza kwamba
lazima wanafunzi wapate elimu bora ili waone umuhimu wa kulipa kodi kwa
maendeleo ya taifa.
“Mazingira bora ya mtoto kupata elimu ni pamoja na kukaa
kwenye dawati… CRDB tumesikitishwa na uhaba wa madawati shuleni hapa hivyo
tumeahidi kuendelea kuwasaidia hasa kipindi hichi cha wiki ya huduma kwa wateja
wetu.
“Tunarejesha asante kwa jamii tunayoihudumia kwa kutuamini,
tumetenda sh bilioni 1.3 tutakazozirejesha kwenu kwa njia mbalimbali, tunasema
asante sana,” alisema Dk. Kimei aliyekubali kuwa mlezi wa shule hiyo.
Asha Mapunda aliyemwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala
na aliipongeza benki ya CRDB kwa kuisaidia serikali kwa njia hiyo huku akikiri
kuwepo kwa uhaba wa madawati katika shule mbalimbali zilizo chini ya ofisi yao.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Maulid Chinyanya baada ya
kuishukuru benki hiyo alimuomba mkurugenzi huyo kusaidia uzio wa shule kwa kuwa
wamezungukwa na makazi ya watu hali inayoondoa umakini wa wanafunzi wakati wa
masomo.
Shule ya msingi Buyuni, Ilala ina walimu 39 wanaofundisha
wanafunzi 2,054 wanaotumia matundu 20 ya vyoo na madawati 398.
No comments:
Post a Comment