Stanslaus Mabula akiongea na wanahabari baada ya kutangazwa mshindi wa Ubunge Jimbo la Nyamagana (CCM)
Na George Binagi-GB Pazzo
Mgombea wa Chama cha Mapinduzi CCM Jimbo la
Nyamagana Mkoani Mwanza ameibuka mshindi wa kiti cha Ubunge katika jimbo hilo
kwa kupata kura 81,017 na hivyo kumbwaga aliekuwa mbunge wa jimbo hilo Ezekiel
Wenje kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema aliepata kura 79,280.
Matokeo hayo yalitangazwa na Msimamizi Mkuu wa
Uchaguzi Jimboni humo ambae pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Tito
Mahinya huku kukiwa na Ulinzi Mkali wa vyombo vya ulinzi na usalama katika
viunga vya ofisi za Jiji hilo.
Akitakangaza matokeo hayo majira ya saa saba usiku wa kuamkia leo, Mahinya alibainisha
kuwa pia CCM imeibuka kidedea kwa upande wa Madiwani ambapo kati ya Kata 18, imeshinda
Kata 14 na Chadema Kata Nne.
Kwa upande wa Wagombea wengine, Chacha Okong’o
(ACT Wazalendo) alipata kura 161, Faida Potea (CUF) amepata kura 1,005, Ahmad
Mkangwa (NRA) kura 104, Mohamed Msanya (Jahazi Asilia) kura 175 na Ramadhan
Mtoro (UDP) amepata kura 68.
Kwa upande wake Mshindi wa Uchaguzi huo
Stanslaus Mabula alisema kuwa tangu awali alitarajia ushindi huo na kwamba suala
la demokrasia limezingatiwa.
Katika hatua nyingine Mabula alibainisha kuwa
atahakikisha anatatua changamoto zinazolikabiri Jiji la Mwanza ikiwa ni pamoja
na kuwaunganisha wakazi wa Jiji katika shughuli mbalimbali za uzalishaji ili
waweze kujitegemea kiuchumi.
Ezekiel Wenje akiongea na wanahabari muda mfupi kabla ya matokeo kutangazwa
Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi Jijini Mwanza Titho Mahinya akitangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu Jijini Mwanza
Kushoto ni Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana akiwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (kulia) muda mfupi kabla ya matokeo kutangazwa
No comments:
Post a Comment