Pages

Friday, October 16, 2015

MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MBAGALA (ACT-WAZALENDO), AHAIDI MAKUBWA KATIKA JIMBO HILO

Mgombea  ubunge Jimbo la Mbagala kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Soud Rajabu

 Mgombea Ubunge Jimbo la Mbagala kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Soud Rajabu (katikati), akizungumza na wanachama wa chama hicho baada ya kumaliza kuhutubia katika mkutano wa kampeni uliofanyika Mbagala Charambe Mianzini Dar es Salaam jana.



Na Dotto Mwaibale

MGOMBEA ubunge Jimbo la Mbagala kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Soud Rajabu ameahidi endapo atachaguliwa nafasi hiyo atahakikisha anapunguza gharama za  huduma za jamii zikiwemo za hospitalini.

Gharama hizo zinahusisha wajawazito wanaokwenda kujifungua kwa kupata mahitaji muhimu kwani hajaona umuhimu wa kwenda na mabegi ya nguo wakati wa kujifungua pamoja na kupunguza foleni kwa asilmia 80.

Akizungumza na wakazi wa jimbo hilo jijini Dar es Salaam wakati wa kampeni zake, Rajabu alisema katika kuboresha afya za wananchi hao atahakikisha anaboresha hospitali zilizopo katika jimbo hilo kutolewa huduma zake zinazofanana na hospitali ya Temeke.

"Ninafahamu mazingira ya watu wa mbagala hivyo nahitaji kutatua kero zenu za barabara, kwa kutanua barabara za mitaa ikiwa ni kuondoa foleni kupungua kwa aslimia 80,"alisema.

Alisema kutokana na kutanua barabara hizo pia atajenga kituo kikubwa cha kisasa cha sanjari na kila kata kuwa na kituo cha afya na kuongeza kuwa kutokana na wananchi wa jimbo hilo kuwa wengi hali ambayo haina uwiano na huduma muhimu kama masoko ataboresha na kuwa la kisasa.

"Soko la Zakhem serikali inasema ni mali yao huku wafanyabiashara wa sokoni hapo wanalipa kodi ya sh.30,000, nikipata nafasi ya ubunge soko hilo litakuwa mali ya umma,"alisema.

 (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

No comments:

Post a Comment