Mkutano wa Mkuu wa Pili wa Chama cha Kudhibiti Mbu cha Pan African (PAMCA) umeingia katika siku yake ya pili jijini Dar es Salaam ambapo watafiti wamewasilisha taarifa zao mbalimbali za utafiti walizofanya katika maeneo yao kutoka nchi mbalimbali za Afrika ikiwa ni pamoja na ushauri wa kitaalam wa kupata suluhisho la kumdhibiti na hatimaye kumtokomweza kabisa Mdudu mbu barani Afrika. Pichani ni Mwanasayansi Mtafiti Kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Dk Bilali Kabula akiwasilisha taarifa yake. Mkutano huo wa siku tatu ulianza Oktoba 6 na utamalizika Oktoba 8, 2015. Imeandikwa na Father Kidevu Blog
Dk Kabula kutoka NIMR aliwasilisha taaifa ya utafiti uliofanywa jijini Dar es salaam kuangalia vinasaba vinavyosababisha usugu wa mbu waenezao Malaria dhidi ya viuatilifu.
Matokeo ya utafiti huo yalionesha kuwepo kwa vinasaba vinavyosababisha mbu wa Malaria kumeng'enya viuatilifu na kufanya kuwa sugu.
Aidha Dk Kabula alisema kuwa na vinasaba vya "KDR" (Knockdown Resistance)vinavyosababisha usugu zaidi ya viuatilifu.
Ili kudhibiti uenezaji wa vinasaba hivyo, ameshauri matumizi ya viuatilifu aina ya organophosphates na carbonates badala ya pyrethroid.
"Dawa nyingi hasa zilizopo nchini ambazo watu huzitumia kupulizia mbu majumbani haziwaui na badala yake mbu hao kuzirai tu kwa muda flani na baade kuzinduka na kuendelea tena na kuuma na kueneza maambukizi ya malaria, hivyo dawa mbadala hazina budi kuanza kutumika kupulizia mbu majumbani," alisema Dk Kabula.
Washiriki wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa leo katika mkutano huo katika siku yake ya pili.
No comments:
Post a Comment