Wachezaji
wa Simba wakishangilia kwa staili ya ‘Selfika’ baada ya Juuko Murshiid kufunga
bao dhidi ya Mbeya City katika dimba la Sokoine jijini Mbeya. (Picha na David
Nyembe)
Kipindi cha kwanza kilianza kwa
kasi huku Simba ikifanikiwa kupata kona katika dakika ya kwanza ya mchezo.
Mlinzi wa kushoto wa Simba
Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ alipiga mkwaju huo ambao ulimkuta Abdi Banda
ambaye aliusukumiza kwa kichwa na kupanguliwa bila mafanikio na mlinda mlango
wa Mbeya City, Juma Kaseja ambapo Juuko Murshiid aliukwamisha nyavu bao lililodumu hadi
mapumziko.
Simba walionyesha uhai zaidi
katika kipindi cha kwanza baada ya kuongoza wakitaka kuongeza bao lingine
ambapo dakika 24 baada ya Mbeya City kushindwa kuitumia vizuri kona waliyopata,
Banda alishindwa kabisa kumalizia kazi nzuri iliyofanywa na safu ya kiungo na
shuti lake kudakwa vilivyo na Kaseja.
Katika dakika ya 18 ya mchezo
Mwinyi Kazimoto baada ya kuwapita viungo wa Mbeya City alijikuta katika wakati
mgumu alipochezewa rafu mbaya iliyomfanya atoe machozi licha ya kadi yoyote
kutotolewa.
Dakika ya 38 ya mchezo huo
uliokuwa wa kuvutia hususani kwa Simba SC walionekana kupiga pasi, Abdi Banda
alionyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea rafu mchezaji wa Mbeya City.
Dakika moja baadaye Kaseja
aliokoa mkwaju uliolekezwa langoni mwake na viungo wa Simba.
Kipindi cha Pili kilianza kwa
kasi ambapo Mbeya City walionekana kuimarika zaidi na kuichezea nusu uwanja
Simba huku ukuta shupavu wa Watoto wa Msimbazi chini ya Hassan Isihaka
ukionyesha umahiri mkubwa kwa kuzuia hatari zote za Mbeya City.
Kwa upande wao mashabiki wa
Simba dimbani hapo walionekana kuwa na furaha muda wote pale camera ya
Wadhamini wakuu wa kurusha matangazo kwa njia ya runinga Azam TV iliyokuwa
ikiendeshwa kwa ‘remote’ ikielea angani huku mashabiki wa Mbeya City wakibaki
kimya.
Aidha mashabiki wa Simba
walionekana kufanya ishara ya ‘mabadiliko’ walipokuwa dimbani hapo hali
iliyowanyong’onyeza mashabiki huku wakiimba ‘Simba! Simba! Simba! Pompo! Eee!
Kidedea! Pompo! Eee! Kidedea! Pompo! Eee! Kidedea!
Aidha mashabiki walivamia
uwanja na kwenda katika basi la Simba kutaka kuwapongeza wachezaji wao kwa
nzuri waliyoionyesha dhidi ya Mbeya City.
Simba walifanya mabadiliko
wakimtoa kipindi cha pili wakiwatoa Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto, Abdi
Banda na kuwaingiza Awadh Juma, Joseph
Kimwaga, Peter Mwalyanzi.
Kwa upande wake Kocha Kerr,
alisifia Mbeya City kwa uimara iliyouoneysha licha ya kuwafunga lakini
alisisitiza kuwa alama tatu kwake ni muhimu na timu yake imelilinda bao lake.
Kocha Mingange alisema makosa
ameyaona, na kwamba walipata nafasi nyingi lakini walishindwa kuzitumia hivyo
wataangalia katika dirisha dogo la usajili ni kwa namna gani wanaweza kukiunda
kikosi vizuri kwa ajili ya ngwe ya lala salama.
Boban
awa kivutio
Licha ya mbembwe nyingi za
mashabiki wa Simba na Mbeya City kabla ya mtanange huo lakini habari kubwa
ilikuwa kumwona kiungo mahiri wa zamani wa Simba, Haruna Moshi ‘Boban’ akiwa
katika uzi wa zambarau na nyeupe kwa udhamini wa RB Battery unaovaliwa na Mbeya
City ambaye alitolewa katika dakika ya 48 akiingizwa Hamad Kibopile.
Hata hivyo alionyesha
uanamichezo pale alifanyiwa ‘sub’ alikwenda kumshika mkono na kumkumbatia
Mwinyi Kazimoto hali iliyoibua shangwe dimbani hapo.
Waikumbuka
17 Oktoba 1993
Simba iliendelea kuwapa raha
mashabiki wake na wapenzi wa kandanda nchini baada ya kuwafumua Atlético
Sportive Aviáco (ASA) ya Angola mabao 3-1 katika dimba la taifa jijini Dar es
Salaam. Mabao ya Simba yalifungwa na Edward Chumila, Abdul Ramadhani ‘Mashine’ na Malota Soma
katika mchezo huo wa awali wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Unakumbukwa kwasababu ya ufundi
ulioonyeshwa siku hiyo ukifanana na dhidi ya Mbeya City jana katika mtanange wa
Ligi Kuu Tanzania Bara.
Vikosi
Mbeya
City
|
Kikosi cha Mbeya City
kilichowavaa Simba SC Okotba 17 , 2015 katika dimba la Sokoine jijini Mbeya.
Simba ilishinda 1-0 Picha na Kenneth Ngelesi)
|
Juma Kaseja, Hassan Mwasapili,
John Kabanda, Yohana Moris, Haruna Shamte, Stephen Mazanda, Christian Sembuli,
Temi Felix, Haruna Moshi ‘Boban’,Joseph Mahundi.
Akiba
Hannington Kasyebula, Hamad
Kibopile, Rajabu Seif, Geofry Mlawa, Seleman Magoma, Richard Peter, Abdala Seif
Coach: Meja Abdul Mstaafu Mingange.
Simba
SC
|
Kikosi cha Simba SC
kilichowavaa Mbeya City Oktoba 17 2015 katika dimba la Sokoine jijini Mbeya.
Simba ilishinda 1-0 Picha na Kenneth Ngelesi)
|
Vincent Angban, Mussa Hassan
Mgosi, Mohamed Hussein, Hassan Isihaka, Murusid Juuko, Justice Majabvi, Said
Hamis Juma, Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto, Abdi Banda.
Akiba
Peter Manyika Jr., Peter
Mwalyanzi, Awadh Juma, Simon Sserunkuma,, Ibrahim Migomba, Pape Ndaw, Joseph
Kimwaga.
Coach: Dylan Kerr
|
No comments:
Post a Comment