![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgGSFjURmDok4KHvLr8qF-wl7aljSBJ7y1zXULJRzp1GjB5mD-_0V9oaAbRcBA0xkdswgovvJZrv4BPVmwrcqQRS4Th3N1TnwCRl-RHdAzH1HLmXNxA3MP5XZ66_FveTiN-yc2L2xhoCr0/s640/ali+kiba+in+action+1.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiS03OaxcbHzyOmiWFaCb9P5gp8li6Ck68IJhx6A_jBsDjoa7MGYkvyOSjxByMntMB3WaVmY-rVpQKzZcd92fkutvWP6LblPu12zVGOD1moICZpwu4gTO3ytvfLDzxpuX8mdiQAEDDWzV8/s640/ali+kiba+in+action+2.jpg)
Mwanamuziki Ali Kiba akionyesha machachari yake katika onyesho la Coke studio akiwa na mwanamuziki wa Kenya Victoria Kimani
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj0k8sc49Ox2rSdiYtkdvMWhrNeFmcR5LOTUooPw6t-t1UtqAWd52RtTPeS0oVcm7NRSq9v012NQKLPwWXvql3Ayz5znP3VzJCfPpCnqJZIYdJqhh5gJeKKECDoQ72jcsk7ZNqVpDAuyq4/s640/ali+kiba+in+action+3.jpg)
Mwanamuziki wa Tanzania Ali Kiba akiwasha moto katika onyesho la Coke studio
Awataka wasanii wachanga kujituma ili
waweze kushiriki kwenye onyesho kama hili
Mwanamuziki nguli wa miondoko ya Bongo Fleva nchini Ali
Kiba amesema moja ya mafanikio anayojivunia nayo katika kazi ya muziki kwa
mwaka huu ni ushiriki wake katika onyesho la Coke Studio msimu wa tatu.
Ali Kiba ambaye amefanya kolabo kwa kushirikiana na
mwanamuziki wa kike anayetamba katika anga ya muziki wa Bongo Fleva nchini
Kenya Victoria Kimani amesema katika mahojiano hivi karibuni kuwa anajivunia
kuwa miongoni mwa wanamuziki wanaoshiriki kwenye msimu wa tatu wa Coke Studio unaoendela ambapo kwa hapa nchini onyesho
hilo linarushwa na luninga ya Clouds kila Jumamosi saa 12 jioni na kurudiwa saa
tatu usiku.
Anasema ushiriki wake kwenye ni bonge la mafanikio
kwani rekodi yake imezidi kuongezeka katika anga la
kimataifa na ameweza kujiongezea washabiki ambao wafuatilia onyesho hili
kupitia luninga,vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
Mbali na kuongelea mafanikio ya kupata washabiki amesema
kuwa amefurahi kufanya kolabo (mash-up) na msanii wa nje ya nchi kwa kuwa
ameweza kujifunza mengi kupitia ushiriki wake kwenye Coke Studio.
Alisema onyesho la Coke Studio linadhihirisha kuwa muziki
wa Bongo Fleva unazidi kukua na kuwa maarufu sehemu mbalimbali barani Afrika
kutokana na jinsi linavyofuatiliwa na idadi kubwa ya watu hususani vijana.
Aliwataka wanamuziki wachanga wanaochipukia kufanya kazi
kwa bidii ili kuhakikisha wanapata mafanikio.
“Fani ya muziki inazidi kukua kiasi kwamba wakati wa
kufanya muziki wa ndani tu imekwisha na inabidi kuvuka mipaka na kufanya
kolabo(mash-up) kama hizi za Coke Studio zinasaidia kupata uzoefu na kufungua
milango ya mafanikio”.Alisema.
Alimalizia kwa kuwapongeza wanamuziki wenzake kutoka
Tanzania ambao wako nao katika msimu wa Coke Studio mwaka huu. Wanamuziki hao
ni Ben Pol ambaye amefanya kolabo (mash-up) na Wangechi kutoka Kenya, Fid Q
ambaye amefanya kolabo (mash-up)Maurice Kirya na Vanessa Mdee ambaye amefanya
kolabo (mash-up) na mwanamuziki 2face kutoka Nigeria.
Onyesho la Coke Studio linarushwa na luninga ya Clouds
kila Jumamosi saa 12 jioni na kurudiwa saa 3 usiku. Pia unaweza sikiliza show
kwenye redio ya Clouds FM kila jumamosi saa 4 asubuhi.
No comments:
Post a Comment