Pages

Saturday, December 19, 2015

BARUA YA WAZI KWA RAIS MAGUFULI

          
Ninayo heshima kubwa kukupongeza kwa kuwa Rais wetu wa awamu ya TANO. Ninayo mambo machache ya kukushauri kama Rais wangu na mimi kama mwananchi wako mpenda maendeleo kama kauli mbiu yako ya hapa kazi tu nayo ni kama ifuatavyo la kwanza ni usafirishaji wa abiria wakati wa usiku badala ya mchana kama ilivyo sasa mimi nakuomba na kushauri turudishe utaratibu wa miaka ya nyuma wa kuruhusu mabasi ya mikoani kusafiri usiku badala ya mchana, hii ni kwasababu. Serikali yetu inapoteza mamilioni ya shilling kwa kuwafanya abiria  wawe safarini mchana mathlani kila siku mabasi yanaondoka DAR yasiopungua 400 kila basi linabeba abiria wasiopungua 60 kwa wastani hii maana kutoka mikoani kuja DAR ni idadi ni idadi kama hiyo hii ina maana kuwa watu wasiopungua 48000 wako barabarani wamekaa iddle hawafanyi kazi, na kama wastani kila mtu  anazalisha TSHS 50,000/= kwa siku  akiwa kazini basi tunapoteza jumla ya shs 2.4
 bilioni kila siku ambazo tungeziokoa kwa kuwasafirisha abiria hao usiku, maana kama nitaondoka Mbeya saa 12 jioni Dsm nitafika saa 12 alfajiri nitafikia kazi tu na jioni naondoka Dsm saa 12 jioni nafika Mbeya saa 12 alfajiri na kwenda kazini asubuhi hiyo hiyo hapa hakuna nguvu kazi iliyopotea maana nimepoteza usiku tu ambao hata hivyo ningekuwa nimelala nyumbani badala yake nitalala kwenye basi ,hii Itaokoa mamilioni ya shilling ya watu na Taifa kwa ujumla


-          Sababu ya pili ni ajali zitapungua sana kwa sababu mchana  kuna joto sana matairi yanapata moto  na hatimaye kusababisha burst na vipuri vya gari kuharibika sana wakati wa mchana kuliko usiku maana injini wakati wa usiku  inapoa nakupunguza   burst za matairi inayosababisha ajali nyingi na hatimaye kupunguza vifo vingi vya watu wetu.
-          Sababu ya tatu ni tutapunguza msongamano uliopo sasa hasa katika miji mikubwa nchini.
-          Sambamba na hilo ili kupungusa ajali kabisa  nashauri malori yapigwe marufuku kusafiri usiku ili yabaki mabasi tu
-          Sababu ya nne ni kwamba nchi nyingi kama sio zote mabasi yanasafiri usiku na hasa ya masafa marefu ninaamini hawa wenzetu waliliona hilo kupoteza nguvu kazi ya watu kwa kuwafanya wasafiri mchana mfano ni Malawi, Zimbabwe, Mozambique , south Africa Namibia n. k najiuliza kwanini nchi yetu iwe kama kisiwa?
-          Sababu ya tano mabasi yatapunguza speed maana atakimbilia wapi sharti afike Dsm asubuhi tu No way out
-          Najua wengi wanafikiri kwamba mabasi yatatekwa hilo kwa sasa halipo kutokana na teknologia ilivyokua maana hayupo mtu anayetembea na hela mkononi tofauti za zamani na hili abiria wengi wanalipenda sana wanashindwa tu pa kusemea, na kutokana hilo abiria wanasafiri usiku na vikosta, Noa na IT ambavyo mara nyingi husababisha ajali ukiacha coasta ,NOA na IT havina balance vinaanguka sana. Ili kumaliza hilo nashauri  serikali yako kuruhusu mabasi ya masafa marefu kusafiri usiku.
-          Nitashukuru sana iwapo utalitazama hili kwa jicho la kiuchumi.
Jambo jingine ninaloshauri ni serikali kuhamia DODOMA  Mh. Rais nitoe mfano wa  nchi jirani ya Malawii ,Rais wa kwanza wa nchi hiyo  Kamuzubanda alianzia makao makuu ya nchi yake kule ZOMBA baadaye akahamia BLANTYRE na baadaye akahamia   LILONGWE kwa nini alifanya hivyo, ni kwa ajili ya kupanua maendeleo katika miji ya nchi hiyo  ambapo  mpaka leo kuna  miji mikubwa Mitatu.

Mh Raisi kama wewe mwenyewe utahami  DODOMA  mkoa utakuwa kwa kasi na kupelekea mikoa ya jirani kukua  kwa kasi kubwa sana
-          Tutapunguziwa safari ndefu za kwenda DAR kufuata huduma za serikali kuu maana DODOMA ilo katikati ya nchi
-          Foleni Dsm itapungua sana kama sio kwisha kabisa
-          Sasa hivi  uchumi wa Tanzaia kwa asilimia 80  unategemea Dsm hebu fikiria ikatokea sunami kama ile ya INDONESIA  je itakuwaje japo hatuombei hilo lakini linaweza kutokea (what if it happen) maana yake tutapoteza uchumi wa nchi kwa 80%.
-          Sambamba na hilo viwanda vitajegwa sana DODOMA na mikoa mingine kuliko ilivyo sasa DSM ndo kila kitu.
-          Mwisho nasema hayo ni mawazo yangu tu yananisumbua kwa muda mrefu sana nimeona kwa kuwa wewe umekuja kwa kauli mbiu ya hapa kazi tu pengine  unaweza ukafanyia kazi haya tukasonga mbele.

Nakuombea kwa Muungu akupe hekima Na busara katika kutekeleza majukumu Mazito ya kuingoza Tanzania.

Wako katika ujenzi wa Taifa.

Andrew Ndingo
0754447501
AMIN

No comments:

Post a Comment