Kwa muda mrefu sasa, kumekuwa na mijadala lukuki kwenye
mitandao ya kijamii kuhusiana na biashara haramu ya madawa ya kulevya. Wapo
wanaharakati na wanasiasa kadha wa kadha wamekuwa wakifanya jitihada za kutaka
kutaja majina ya walio nyuma ya biashara hii, lakini mwishoni hupatwa na
kigugumizi na kuishia hewani.
Marehemu Amina Chifupa (MB), aling'aka bungeni na kutangaza
kwamba anayo majina ya wanaojihusisha na biashara hii haramu na atayataja muda
wowote, lakini kwa bahati mbaya akatangulia mbele ya haki kabla ya kutimiza
azma yake hiyo.
Rais mstaafu wa awamu ya nne ya JMT, Mhe. Jakaya Kikwete
alinukuliwa akisema amepatiwa majina ya watu wazito wanaojihusisha na biashara
hiyo, lakini naye mpaka anaondoka madarakani, hakuchukua hatua zozote.
Yupo Blogger Mtanzania aishiye ughaibuni anayeitwa Mange
Kimambi, naye amekuwa mstari wa mbele kupiga kelele kuhusu vigogo
wanaojihusisha na biashara ya madawa ya kulevya inayoangamiza vijana wengi na
kuharibu nguvukazi ya taifa, lakini mpk sasa Jeshi la Polisi na vyombo vya
usalama nchini vinaonekana kusua sua kulivalia njuga suala hili.
Leo, gazeti la Jamhuri limeandika orodha ya majina ya
wanaohusishwa na biashara hii ya madawa ya kulevya ambayo yamekabidhiwa kwa
waziri wa mambo ya ndani, Mhe. Charles Kitwanga ambaye ameyafikisha kwa
Mheshimiwa John Pombe Magufuli (kwa mujibu wa gazeti hilo).
Je, hii inatoa ishara njema ya 'kutumbuliwa jipu' hili la
muda mrefu?
No comments:
Post a Comment