Pages

Wednesday, December 23, 2015

Hospitali ya ApolloYatoa “Zawadi ya Maisha” kwa Kufanikisha Upandikizaji wa Moyo na Ini kwa Kijana wa umri wa Miaka 30

 Ponnar, kijana aliyefanyiwa upandikizaji wa Moyo na Ini kwa pamoja, katika hospitali ya Apollo akizungumza na waandishi wa habari baada ya upandikizaji huo.
Ponnar, kijana aliyefanyiwa upandikizaji wa Moyo na Ini kwa pamoja, akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa hospitali ya Apollo baada ya upandikizaji. Aliyemkumbatia  ni  Mwenyekiti na Mwanzilishi wa hospitali za ApolloDk. Prathap .C. Reddy.


Na Mwandishi Wetu,
Hospitali za Apollo zimefanikiwa kwa mara ya kwanza barani Asia kufanya upandikizaji wa moyo na ini; hivyo kujiunga na timu ya hospitali chache duniani zilizowahi kufanya upasuaji huo wa aina yake.
Desemba 2015; Hospitali za Apollo ambazo ni kinara barani Asia kwa ubora wa huduma za afya, kwa mara nyingine zimeonyesha ubora wake wa uongozaji kupitia kituo cha upandikizaji duniani kwa kufanikisha upasuaji wa upandikizaji kwa mpigo wa ogani za moyo na ini  kwa kijana mwenye umri wa miaka 30 anayetokea Tiruchengode, Tamilnadu nchini India. Tukio hilo linalotambulika kitaalam kama en-Bloc CHLTni mfumo mgumu wa upasuaji na haujawahi fanyika popote barani Asia. Kama ilivyoitwa na chuo cha Stanford kuwa ni “upasuaji wa kiufundi na kitaalam sana, ambao ni vyema uachwe kwenye mikono ya madaktari bingwa wenye ujuzi”, ni hizo hatua za CHLT pekee zimeweza kufanyika ulimwenguni pekee.

 
Stori hii ya Ndg. Ponnar, kijana mtulivu kutokea Tiruchengode, mji mdogo kutokea wilaya ya Namakkal Tamilnadunchini India. Ponnar alikuwa ni mwanafunzi bora aliyemaliza stashahada yake kwenye fani ya uhandisi na alikuwa na medali ya dhahabu. Katika umri wa miaka 22, kama kijana mwenye malengo makubwa na matumaini ya kufikia ndoto zake, Ponnar alianza kuhisi kujaa maji tumboni mwake, upungufu wa pumzi na kujikuta rangi ya ngozi yake kuanza kuwa manjano.
Hii ilitambulika kama kufeli kwa ini, iliyopelekea kufanyiwa kwa upandikizaji wa ini, ambao familia yake ilikuwa tayari kwa kijana huyo kufanyiwa hilo zoezi la upandikizwaji.  Wakati alipofika kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji huo wa kupandikizwa ini, iligundulika kuwa Ponnar anatatizo katika mfumo wa upumuaji unaoitwa kitaalam Ebsteins anomaly au kufeli kwa upande wa kulia wa moyo katika kufanya kazi kwa usahihi ambao ndio awali umeletea udhoofu katika ini.
Bahati mbaya kujumuika kwa matatizo mawili kwa mpigo kulimfanya Ndg Ponnar kutokuwa na njia mbadala yoyote mbali na kujumlisha upandikizaji wa  ini na moyo. Hii ni hatua ya upasuaji inayohusisha njia kuu mbili  kwanza ya kupitia kooni na kifuani (kwa ajili ya moyo) na kupitia tumboni (kwa ajili ya ini) hivyo kufanya zoezi kuwa hatari sana.
Ponnar- kwa utulivu na ukakamavu alijiandaa kupigania uhai wake mpaka mwisho. Familia yake hasa dada yake ambaye alikuwa tumaini na nguzo kwake, maamuzi ya kwamba watafanya lolote liwezekanalo kuhakikisha wanamwokoa kijana wao, walimpelekea hospitali za Apollo, Chennai, India.
“kwa tatizo la kuwa na moyo usiofanya kazi ipasavyo, kulikuwa na presha kubwa upande wa nyuma wa ini iliyosababisha kuharikika kwa seli za ini iliyopelekea udhoofu huo wa ini. Kwa kuongezea, timu ya upandikizaji wa ogani walijadili uwezekano mkubwa wa uvujaji mwingi wa damu hasa kwa kuwa ni upasuaji wa sehemu mbili kwa mpigo na pia uwezekano mkubwa wa sumu kujikusanya kwenye ini, kuathiri moyo hasa kama ogani hizo mbili zitapandikizwa tofauti tofauti” alisema ”Dk. Paul Ramesh, mshauri mwandamizi wa upasuaji katika mfumo wa upumuaji kutoka hospitali za Apollo, Chennai.
Upasuaji na upandikizaji wa moyo na ini unaweza fanyika kwa njia kuu tatu;
1.    Kwanza upandikizaji wa moyo- ufuatiwe na upandikizwaji wa ini pale mgonjwa atapokuwa amepata nafuu kutokana na upasuaji wa kwanza.
2.    Kwanza upandikizwaji wa moyo- ufuatiwe na upandikizwaji wa ini kama njia mbili tofauti ila kwa mpigo katika operesheni moja.
3.    Upandikizwaji wa moyo na ini kwa pamoja, inafanyika kwa ogani zote kuchukuliwa kama moja na kupachikwa kwa pamoja kwa mpigo.
Ni wale mabigwa tu kwenye ile timu ya upandikizwaji wa ogani kufanya kazi pamoja kama timu moja na kuleta matumaini ya kufanikisha en-bloc CHLT mfumo adimu sana kufanyika duniani.
”kwa zaidi ya miongo ya ujuzi katika upandikizwaji wa ogani, imetuwezesha kupata maarifa na utaalamu unaohitajika kufanya  operesheni ngumu kama hizi. Mafanikio yetu katika upandikizwaji wa moyo na ini yaliyopatikana yametupatia msingi na uimara katika uendeshaji bora wa en-bloc CHLT kwa bara la Asia. Najivunia sana kwa ajili ya Ponnar na familia yake walioweza kuimanini timu kutoka hospitali yetu ya Apollo, imetupa sana motisha sisi kuendelea mbele na mfumo huu bila mipaka ili kufika juu kabisa. Aliongeza Dk. Ramesh.
Ponnar alisubiri kutokea April hadi 0ktoba 2015 ili mtoaji damu anayemfaa alipopatikana. Alifanyiwa upasuaji wa upandikizwaji huo wa moyo na ini tarehe 14 oktoba 2015 na aliruhusiwa kwenda nyumbani ndani ya wiki baada ya upasuaji huo. Leo hii, Ponnar ni mzima wa afya njiani kuelekea kupona kabisa na kurudia maisha yake ya awali- ni mwenye furaha sababu ngozi yake sio ya njano tena, na sasa anaweza kuendelea kufurahia raha za maisha kama kutembea kwa miguu yake mwenyewe. Kwa maumivu yaliyokuwa nyuma kwa miaka 8, sasa Ponnar yupo huru kuendeleza matumaini yake na ndoto zake.
Ngazi hii ya kimatibabu, ya upandikizwaji wa moyo na ini kwa mpigo (mara ya kwanza barani Asia) ni hazina kubwa kwa Ndg Ponnar na dada yake,walioweza kutosikiliza uzushi wa watu wote. Pia ni ushuhuda kuwa timu ya madaktari wa upandikizwaji kutoka hospitali za Apollo Chennai wamefanikiwa kufanya operesheni hii kwa mafanikio makubwa. Haya yote yasingeweza kufanikiwa kama pia kusingekuwepo kwa ushirikiano mkubwa kutoka serikali ya Tamilnadu na programu ya kujitolea ogani iliyopo Tamilnadu ambayo imesifiwa ulimwenguni kwote kwa kazi kubwa walioifanya.
”mafaniko haya makubwa ni agano kwa mabingwa wote wa upasuaji duniani, madaktari, wataalam, manesi na wafanyakazi wote waliojitolea kuwahudumia wagonjwa na kutoa huduma zilizopo katika viwango vya kimataifa. Upasuaji ni matokeao ya mipango bora iliyofanywa kwa siku kadhaa kutoka kwa timu ya wataalam upande wa moyo na ini na uonekanaji wa miundo mbinu bora na wataalam waliokubuhu. Jitihada hizi shirikishi zinachukua timu zote za upandikizaji ili kutathimini na kuweka mikakati kasha kuonyesha kuwa fani hii ni ya kuheshimika”. Alisema Dk. Prathap C Reddy, mwenyekiti na mwanzilishi wa Hospitali za Apollo
Kuhusu Hospitali za Apollo
Hospitali ya Apollo ilifunguliwa mnamo mwaka 1983, na kutoka kipindi hicho imekuwa ikiendeshwa kwa kauli mbiu isemayo "Dhamira yetu ni kuleta huduma ya kisasa karibu kabisa na walengwa. Tunajitolea kutoa huduma bora na mafanikio katika elimu na  utafiti kwa ajili ya jamii  ya kibinadamu".Katika miaka 30  tokea kuanzishwa kwake, hospitali ya Apollo imeandika historia kubwa kupata kuonekana nchini India. Ni moja ya kampuni kubwa ya Afya katika bara la Asia, na pia imeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya afya nchini india.
Katika safari yake, imeweza kuboresha maisha ya watu wapatao milioni 39 kutoka nchi 120.Inatoa huduma maalum 52 na vitanda vya upasuaji 710.Imefanya upasuaji wa moyo wenye kufikia idadi ya watu 152,000 na panuzi 125, 000 za mishipa myembamba.Imefanya upasuaji wa wa viungo unaopita kiasi cha idadi ya watu 10,000, upasuaji wa uvimbe wa ubongo, uti wa mgongo na zaidi.Taasisi ya Apollo ni moja ya taasisi zinazoongoza nchini india, zikiwa na teknolojia za kisasa kama Novalis TX, PET MRI na Upasuaji unaotumia mashine za kiroboti.

No comments:

Post a Comment