Meneja wa klabu ya Chelsea ya
Uingereza amefutwa kazi baada ya klabu hiyo kuandikisha msururu wa matokeo
mabaya. The
Blues walishinda Ligi ya Premia msimu uliopita lakini msimu huu mambo yamekuwa
kinyume, na wamo alama moja tu juu ya eneo la kushushwa daraja ligini. Bodi ya
klabu hiyo ilikutana jana kujadili hatima ya Mourinho chini ya mmiliki wa klabu
hiyo, Mrusi Roman Abramovich.
Klabu hiyo kupitia
taarifa imesema mkataba kati ya klabu na meneja hiyo umekatishwa kwa maelewano
kati ya pande zote mbili na ikamtakia kila la kheri Mourinho.“Sifa zake
Stamfrod Bridge na Uingereza zinajieleza na daima anakaribishwa kurejea
Stamford Bridge,” klabu hiyo imesema kupitia taarifa.
“Sasa tutaangazia
kuhakikisha kikosi chetu kilichojaa wachezaji wenye vipaji kinafikia uwezo
wake. Hakutakuwa na taarifa zozote zaidi kutoka kwa klabu hadi kocha mpya
ateuliwe.”
No comments:
Post a Comment