Headlines za mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga katika klabu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mbwana Samatta zinazidi kushika kasi, Samatta
anatajwa kuwa katika mpango wa kwenda kucheza soka la kulipwa barani
Ulaya,mara tu dirisha dogo la usajili la mwezi January
litakapofunguliwa.
Headlines ambazo zimenifikia kutoka katika mtandao wa www.voetbalkrant.com zinaripo nyota huyo tegemeo wa watanzania kuwa katika mipango ya kwenda kucheza soka katika klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji, Samatta anatajwa kuandikwa na mitandao ya Ubelgiji kujiunga na klabu hiyo.
Samatta ambaye anatajwa kuwa na rekodi ya kucheza jumla ya mechi 103 na kufunga jumla ya magoli 60 toka ajiunge na TP Mazembe mwaka 2011 kwa mujibu wa www.voetbalkrant.com, anatajwa uwezo wake kumvutia mkurugenzi wa ufundi wa klabu ya KRC Genk Dimitri De Conde.
KRC Genk ambayo msimu
huu inatajwa kuwa na safu mbovu ya ushambuliaji, mwaka 2012 ilishiriki
na kuingia katika hatua ya makundi ya michuano ya klabu bingwa Ulaya,
klabu ya KRC Genk (Racing Genk) ndio klabu iliyomuuza kiungo wa sasa wa Man City Kevin De Bruyne na golikipa namba moja wa sasa wa Chelsea Thibaut Courtois kwenda Chelsea mwaka 2012. Kwa sasa klabu hiyo ipo nafasi ya sita katika msimamo wa Ligi Kuu Ubelgiji.
No comments:
Post a Comment