Professor Jay
ni mwana Hiphop kitambo sana hapa Tanzania, lakini jina lake lina uzito
wake wa nguvu kabisa kiasi cha kwamba watoto, vijana, wazee na watu
wazima walilifahamu jina lake… lakini 2015 inamalizika huku akiwa na
kofia nyingine kichwani, ni kofia ya Ubunge wa Jimbo la Mikumi Morogoro a.k.a Mji kasoro bahari !!
Prof. Jay kaanza kazi na kathibitisha kwamba ndani ya siku 20 anaweza kufanya kitu na kikaonekana… nakumbuka Mbunge huyo, Joseph Haule alikuwa mmoja ya Wabunge walioapishwa siku ya November 18 2015 Bungeni Dodoma.
Kazi imeanza, amenithibitishia kwamba
ameanza na ukarabati wa barabara kati ya Kata ya Kidodi na Kata ya
Vidunda ambapo barabara hiyo itakuwa kwenye hali nzuri ya kupitika
tofauti na hali ilivyo sasa, imeharibika vibaya kutokana na mvua.
Kingine ni kwamba Professor Jay
amesema kipaumbele chake ni kwenye mambo manne makubwa, kuhakikisha
upatikanaji wa maji, ukarabati wa barabara, uboreshaji wa elimu na
huduma bora za afya… barabara aliyoanza nayo kwa sasa ina umbali wa kama
kilometa saba hivi.
No comments:
Post a Comment