Mizigo ikipakizwa kutoka kwenye nyumba hiyo.
Musa Mateja
UFALME
umeanguka! Unaweza kusema hivyo! Hatimaye Miss Tanzania 2006, aliye pia
staa wa filamu za Bongo, Wema Isaac Sepetu amedaiwa kutimuliwa kwenye
nyumba ambayo alipanga kwa mbwembwe na kualika waandishi wa habari ili
watoe ‘nyuzi’ hewani, akidai ni yake kwa kuinunua kwa shilingi milioni
280, fuatana na Ijumaa Wikienda.
Kwa mujibu
wa chanzo chetu makini, Wema amekumbwa na kadhia hiyo ya kuhamishwa
kwenye nyumba hiyo iliyopo Makumbusho jijini Dar, usiku wa Desemba 18,
mwaka huu.
SIKIA CHANZO
“Jamani
mmesikia kilichomtokea Wema Sepetu? Yaani huyu dada anaishi kwa maigizo
hadi basi. Lile sakata lake la kudaiwa kutumia umeme na maji kimagumashi
limemtokea puani, maana kwenye umeme pekee yake nasikia anadaiwa zaidi
ya shilingi milioni nane (8,000,000) fedha ambazo imekuwa shida kulipa.”
Mizigo ikiwa kwenye gari.
BABA MWENYE NYUMBA AINGIA KATI
“Sasa baba
mwenye nyumba ameingilia kati. Ameamua kulipa yeye deni hilo lakini
akamtaka Wema ahame haraka kwenye nyumba yake,” kilisema chanzo.
SIKU YA TUKIO
Paparazi
wetu alizidi kupenyezewa ‘ubuyu’ kuwa, muda huo tayari kuna lori aina ya
Toyota Canter linahamisha vitu nyumbani kwa Wema na kwamba, kuna kila
dalili anahama baada ya baba mwenye nyumba wake kumtimua.
PAPARAZI NYUMBANI KWA WEMA
Ilibidi
paparazi wetu akimbie kwa pikipiki iendayo kasi mpaka nyumbani hapo na
kukuta kweli lori likibeba vitu mbalimbali huku wabebaji wakitokwa jasho
chapachapa.
Gari hilo lilisimama kwenye lango kuu la kuingilia ndani ya nyumba hiyo huku likiwa na shehena ya mafurushi ya mizigo.
Muonekano wa mjengo huo.
Wakati
paparazi wetu akiwa kwenye hali ya mshangao, aliendelea kuona mizigo
mbalimbali ikitoka ndani ya mjengo huo huku vyombo anuai vya ndani, kama
kabati na baadhi ya makochi yakiwa nje ya nyumba hiyo yakisubiri
kupakiwa tayari kwa safari ya kumuondoa Wema kwenye mjengo huo.
WEMA HAYUPO
Swali la kwanza kwa wabebaji hao kutoka kwa paparazi wetu ni wapi alipo Wema.
“Unamtaka Wema wa nini wakati unajua hayupo hapa, kwanza wewe nani?” alikuja juu mpakiaji mmoja.
Vitu vikiwa nje.
PAPARAZI ANUSURIKA KIPIGO
Katika hatua
nyingine isiyokuwa ya kawaida, wapakiaji wengine walitaka kumshushia
kipigo paparazi wetu baada ya kuona mwanga wa kamera wakati akichukua
picha kadhaa kwa ajili ya ushahidi.
WALIKOHAMIA
Uchunguzi wa
awali, Wema amehamia Mbezi Beach, Dar. Hata hivyo, tangu sakata la wizi
wa maji na umeme, Wema hajawahi kulala na kuamka ndani ya nyumba hiyo
huku habari zikisema amekuwa akiishi mahotelini kama ‘digidigi’.
KWA NINI WEMA ALISEMA NYUMBA NI YAKE?
“Kuna watu
wengi walikuwa hawatambui kwa nini Wema awali alisema hii nyumba ni
yake. Mwanzo wakati anahamia, pia alikuwa ana mazungumzo na baba mwenye
nyumba kwamba ainunue lakini watoto wakagoma hivyo Wema akawa analipa
kodi kila mwaka.
WEMA, PETIT MAN
Juzi, Wema
hakupatikana hewani ili kujibu madai hayo, lakini mmoja wa watu wake wa
karibu, Petit Man alikumbana na paparazi wetu katika klabu moja jijini
Dar, alipoulizwa kuhusu mambo hayo alikiri Wema kuhama kwenye nyumba
hiyo.
“Tena sasa tunahamia kwenye nyumba aliyonunua Wema mwenyewe. Bonge la nyumba, mtaipata habari yake. Iko Mbezi Beach,” alisema Petit.
Source:Global Publishers
No comments:
Post a Comment