Waziri
wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye(kushoto) akiongea
na Mchezaji wa Timu ya TP Mazembe Mbwana Samatta(kulia) jana jijini Dar
es salaam.Mbwana amemtembelea waziri Nape ofisini kwake na kuomba
baraka za wizara katika kinyanganyiro cha kugombea uchezaji bora wa
afrika anayechezea ligi za ndani na pia kumpa habari njema za yeye
kutegemea kujiunga na timu ya Ubelgiji ya Genk.
Waziri
wa Habari,Utamaduni,sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye(katikati)akiongea
na waandishi wa Habari na kuwaomba watanzania kumwombea Mbwana Samatta
ili ashinde katika kinyanganyiro cha kugombea uchezaji bora wa afrika
anayechezea ligi za ndani kwani ni jambo la Taifa zima.Mhe Nape pia
alimhakikishia kuwa Serikali ipo nyuma yake na ipo katika mkakati wa
kuifanya michezo kuwa Shughuli Rasmi kwani itawafaidisha wanamichezo na
Serikali kwa kupata kodi.
Mchezaji
wa TP Mazembe Mbwana Samatta(wa kwanza kushoto)akiongea na waandishi wa
habari(hawapo pichani) sababu za yeye kumtembelea Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo katika ofisi ya Wizara hiyo.Mbwana
alisema kuwa amemtembelea waziri uyo kwa ajili ya kumfahamisha kuwa
yumo katika kinyanganyiro cha kugombea uchezaji bora wa afrika
anayechezea ligi za ndani na hivyo kuomba baraka za Wizara.Pia
kumpongeza Mhe. Nape kwa kuchaguliwa kuwa waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.Mbwana anategemea kujiunga na klabu ya
Mpira ya Genk ya Ubelgiji kwa mkataba wa miaka minne.
Picha na Daudi Manongi-WHUSM.
No comments:
Post a Comment