Pages

Thursday, January 21, 2016

MAJIBU YA MKWASA KUHUSU CANNAVARO KUSTAAFU KUICHEZEA TAIFA STARS


Charles Boniface Mkwasa, Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania
Charles Boniface Mkwasa, Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania
Siku kadhaa baada ya nahodha wa muda mrefu wa Stars Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kutangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa ‘Taifa Stars’, hatimaye kocha mkuu wa kikosi hicho Charles Boniface Mkwasa amesema hajapata taarifa rasmi na kuongeza kuwa, Cannavao bado yupo kwenye mipango yake ya timu ya taifa ya Tanzania.“Mimi nafikiri si vizuri kuzungumza kwasababu nimekuwa nikizungumza muda mrefu na nikizungumza tutazidi kuchochea, mimi nafikiri maamuzi yatakuwa yamebaki kama nilivyozungumza”, amesema Mkwasa.

 
“Ninaheshimu maamuzi ya Cannavaro, ni mchezaji mzuri nimekaanaye ni kongozi mzuri anahamasisha vizuri na bado mimi namuhitaji. Lakini nilichokifanya ni mabadiliko ya kawaida tu kwenye timu kwakuwa yeye niliamini anaweza kuwaongoza watanzania kwenye mashindano ya CHAN na nilimpa taarifa mapema lakini sasa sitaki kulumbana nafikiri hivyo ndivyo itakuwa imebakia”.
“Nimshauri kwamba, bado anahitajika na nasikia kwenye vyombo vya habari kwamba amestaafu lakini bado mimi sitambui kustaafu kwake. Hata kama kustaafu lazima astaafu kwa heshima na lazima tufanye utaratibu na mimi nitasimamia utaratibu wake ili tuweze kuandaa atastaafu vipi”.
“Nisingeweza kuandaa sasahivi kwasababu hatuna program ya national team, tutakapokuwa na program ya national team basi tutafanya utaratibu kwa kukubaliana naye na kumwambia kitu gani sisi tumekusudia”.
“Lakini mimi namuheshimu na bado namuhitaji kama atahitajika”, alimaliza Mkwasa.
Cannavaro alitangaza kustaafu soka la kimataifa akipinga utaratibu uliotumika kumvua kitambaa cha unahodha na kumkabidhi Mbwana Samatta. Cannavaro alisema yeye kama nahodha hakupewa taarifa rasmi ya kubadilishiwa majumumu zaidi ya kupata raarifa hiyo kupitia vyombo vya habari, hivyo kwake ilikuwa ni kudharauliwa.

No comments:

Post a Comment