Pages

Tuesday, January 5, 2016

MAKAMU WA RAIS MHE SAMIA AWASILI MKOANI GEITA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa Geita Mhe. Fatma Mwassa wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa GGM Mkoani Geita Januari 04,2016 kwa ajili ya kuanza ziara ya siku mbili ya kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo Mkoani humo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na baadhi ya wawekezaji wa Mgodi wa GGM Mkoani Geita alipowasili Uwanja wa ndege wa GGM Geita Januari 04, 2016 kwa ajili ya kuanza ziara ya siku mbili ya kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo Mkoani humo. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza katika kikao cha kupokea Taarifa ya Maendeleo ya Mkoa wa Geita, kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo,  Januari 4, 2016.

 
Mkuu wa Mkoa Geita Mhe. Fatma Mwassa akizungumza wakati akitoa Taarifa ya Maendeleo ya Mkoa wa Geita, kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia), katika kikao kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo, Januari 4, 2016. Katikati ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Injiani Gerson Lwenge.
Msemaji wa Mkuu wa Kampuni ya Geita Gold Mining (GGM) ambao ni wadau wakuu wa Maendeleo mkoa wa Geita, Tenga Tenga akifatilia kwa makini Hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, katika kikao kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo,  Januari 4, 2016. 
Sehemu ya Watumishi mbali mbali wa vyama na Serikali wa Mkoa wa Geita, wakiwa kwenye kikao hicho.


PICHA NA OTHMAN MICHUZI, GEITA.

No comments:

Post a Comment