Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza (CCM) Stanslaus Mabula akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo
Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza Stanslaus Mabula (CCM,
ameahidi kushughulikia suala la ujenzi wa maegesho ya magari makubwa ya mizigo
nje ya jiji la Mwanza ili kuzuia magari hayo kuingia katikati ya jiji.
Akizungumza ofisini kwake hii leo, Mabula amebainisha kuwa upo mpango wa
kujenga maegesho hayo katika maeneo yaliyo nje ya Jiji la Mwanza, hatua ambayo
itasaidia magari hayo kutoingia katikati ya Jiji na hivyo kuondoa malalamiko
yaliyopo kutoka kwa madereva wa magari madogo ya mizigo wanaolalamikia uingiaji
wa magari makubwa ya mizigo katikati ya jiji.
Ameyataja maeneo yanayotarajiwa kujengwa maegesho hao kuwa ni Buhongwa
pamoja na Igoma na kwamba baada ya ujenzi wake kukamilika, magari yote makubwa
ya mizigo hayataruhusiwa kuingia katikati ya Jiji.
Mabula ambae alikuwa Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza katika uongozi
uliomalizika mwaka jana, amebainisha kuwa utekelezaji wa ujenzi wa maegesho
hayo unatarajiwa kufanyika kwa uharaka zaidi ambapo amewahimiza wawekezaji
mbalimbali kujitokeza ili kushirikiana na halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa
ajili ya kufanikisha ujenzi huo.
Suala la magari makubwa kuingia katikati ya Jiji la Mwanza huku yakiwa
na mizigo, linalalamikiwa na madereva wa magari madogo ya mizigo kwa kile
wanachoeleza kuwa wanaingiliwa katika shughuli ambazo wao wangezifanya na hivyo
kujiingia kipato ambapo wameiomba halmashauri ya Jiji la Mwanza kutoruhusu
magari hayo kuingia katikati ya Jiji.
Bonyeza PLAY Hapa chini Kusikiliza
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza (CCM) Stanslaus Mabula akiongea na wanahabari ofisini kwake.
No comments:
Post a Comment