Pages

Wednesday, January 20, 2016

Muujiza wa Kupandikizwa kwa Uboho (Bone Marrow) Ulivyobadilisha Maisha

The founder and Chairman of Apollo Hospitals Dr. Prathap .C. Reddy.

Mara nyingi watu kutoka nchi zilizoendelea waishio na tatizo la damu na upungufu wa kinga mwilini huishi, tofauti na nchi zinazoendelea ambazo zinakumbana na uhaba wa huduma ya kupandikiza uboho.
Huduma za kisasa na bora za kupandikiza uboho katika nchi zinazoendelea kama Tanzania bado ni tatizo; kusubiria huduma bora katika nchi hizi zinazoendelea, inaendelea kuhusiana na hali mbaya ya kiafya na vifo. Hii ni kutokana na ripoti mpya za kiafya. Kutokana na takwimu za mwaka 2012, ni nchi tatu tu za kiafrika ambazo ni Misri, Afrika kusini na Nigeria ambazo zina hospitali zenye uwezo wa kupandikiza uboho.
Upandikizi wa uboho ni njia mpya ya kisayansi na udaktari 

 
katika kutibu matatizo na maradhi kama Leukimia, kuvimba kwa seli (Lymphoma), saratani katika seli nyeupe (Multiple myeloma), sicko seli anaemia, kuharibika kwa uboho (Aplastic anaemia), Thalassemia, ukosefu wa seli nyeupe (Congenital neutropenia), na upungufu wa kinga za mwili. Matatizo maalum kama ya uvimbe na ulemavu wa kurithi kama Thalassemia pia umepatiwa ufumbuzi mzuri kupitia matibabu haya.
Upandikizwaji wa uboho na seli za mfumo wa kati wa damu ni mfumo unaorudisha seli katika shina la mfupa zilizoharibiwa kwa matumizi makubwa ya mionzi ya kuulia saratani na mionzi mingine pia. Baada ya kupatiwa tiba kwa dozi yenye nguvu ya dawa za saratani na mionzi, mgonjwa huwa anatengeneza shina bora la seli, zinazo safiri kwenye uboho na kuanza kutengeneza seli mpya za damu.
Kwa mujibu wa daktari mtaalamu wa upasuaji Tanzania Dk. Harrison Chuwa, upandikizwaji wa uboho ni wa muhimu sana kulinganisha na madhara ya kutokufanya hivyo kama kupata magonjwa ya leukaemia, seli kuvimbiana hasa kwa kesi za kupooza kwa viungo vya mwili.
“Upandikizwaji wa uboho ndio tiba ya mwisho kwa wagonjwa wenye saratani ya damu,watanzania wengi huwa wanapewa rufaa ya kwenda kufanya upandikizwaji katika hospitali za Apollo India kwa kudhaminiwa na wizara ya afya na ustawi wa jamii” Alisema Dk. Chuwa.
Ufanano katika uboho au seli za damu unaokusanywa kutoka kwa wanaojitolea damu kwa wagonjwa wanaohitaji inaweza kuokoa maisha ya wagonjwa zaidi ya asilimia 70.
Wastani wa gharama za kufanya upandikizaji wa uboho kwa nchi zilizoendelea ni kati ya dola za kimarekani 50,000 mpaka dola 1,000,000 kulingana na aina ya hospitali unayofanyia. Kwa nchi kama Singapore, Malaysia, Brazil, Mexico, India, Thailand, Hong Kong gharama ni kati ya dola za kimarekani 20,000 mpaka 60,000 kulingana na aina za hospitali.
Kwa mujibu wa www.patient-help.com, Marekani na Ulaya wanatoa huduma ya gharama zaidi ya upandikizwaji wa uboho kwa dola 200,000 na upandikizwaji kwa kupata mtoaji damu anayefanana na kundi lako ni dola 250,000. Hii ni tofauti na India ambao wanatoa huduma hiyo ya kwanza kwa dola 35,000 na ya pili kwa dola 50,000.
Mbali na kupewa cheti kutoka JCI hospitali za Apollo nchini India zinatoa matibabu bora kabisa kwa kutumia vifaa vya kisasa na kwa bei nafuu kulinganisha na mataifa ya Ulaya na Marekani. Kutokana na uhitaji wa upandikizwaji wa uboho duniani kote, hospitali za Apollo zimezindua huduma maalum ya upandikizwaji wa uboho. Kitendo hicho kimeifanya hospitali hii kuwa kitengo cha kiteknolojia katika afya bora.
Hospitali za Apollo zilifungua milango yake mwaka 1983 na kutambulisha huduma bora za kimataifa nchini India, kwa gharama zilizo chini sana kulinganisha na zile za ulaya. Hii ni mara ya kwanza kwa hospitali za Apollo kuchukua jukumu kubwa hilo la kiafya na kuifanya kuwa hospitali kubwa ya kwanza kutumia teknolijia ya hali ya juu katika matibabu”. Aliyasema hayo mwanzilishi na mwenyekiti wa hospitali za Apollo Dk. Prathap.C. Reddy.
Kituo cha upandikizwaji wa uboho katika hospitali za Apollo, kimefanikiwa kufanya zaidi upandikizaji 700 kwa mafanikio ya hali ya juu. India ni nchi inayosifika kwa upandikizwaji kwa wagonjwa wanaotoka mataifa mbalimbali, kwa sababu sio tu kwa kwamba hospitali hizi zina timu za madaktari bingwa wa upandikizaji bali pia wana njia nyingi bora za kuzuia madhara ya kiafya katika zoezi hilo.
Tanzania ni kati ya nchi iliyonufaika na vituo vya afya kutoka hospitali za Apollo. Katika mahojiano siku za karibuni na mgonjwa aliyetambulika kwa majina ya Dk. Philip Robert Hiza ambaye baada ya kugundulika ana tatizo la seli alipewa rufaa kwenda hospitali za Apollo ambapo alipatiwa matibabu kwa miezi mitano yanayohusisha upandikizwaji wa uboho pia, Dk. Philip Robert Hiza alikiri kuwa upandikizwaji wa uboho umeleta mafanikio makubwa katika maisha yake.
Maendeleo haya katika matibabu yamepunguza kiwango ha muda uliokuwa unatumika hospitalini kwa ajili ya mgonjwa kupata nafuu. Na kupata nafuu ndani ya muda mfupi kunapunguza gharama za matibabu pia.

No comments:

Post a Comment