MAKALA YA TEZI DUME
(Kutoka kwa Dr. Mackfallen Giliard)
Kwa kawaida mwanaume ana matezi mawili yanayohusiana na
uzazi. Tezi la kwanza linaitwa cowper's gland
Kazi ya hili tezi ni kutoa majimaji ya kuondoa acid
iliyoachwa kwenye njia ya mkojo na mkojo. Kwa wanaume wanajua hivi ni vile
vimajimaji vinavyoaanza kabla ya kuja mzigo wenyewe
Hii inatokana na ukweli kuwa mbegu za kiume zinaishi kwenye
mazingira ya Alkali. Tezi la pili ni Prostate.
Kama linavyoonekana hapo kwenye picha hapo juu hili tezi
lipo kwenye shingo ya njia ya mkojo. Kwa hiyo basi tezi hili likileta mishkeli
tu kidogo linaziba njia ya mkojo na mtu kushidwa kukojoa. Kazi ya hili tezi ni
kutoa majimaji kwa kikwetu tunaita Shahawa. Huu ute mzito una kazi kuu mbili.
Kazi ya kwanza ni
kuwezesha mbegu ziweze kuogeleaaa na kubembeaa na kazi ya
pili ni kuondoa hali ya acidi kwenye uke na kuweka hali ya Alkali (hii ndio maana
tukaita chumvini shauri ya acid) kwani mbegu zinaweza kuishi kwenye acid.
Kwa kawaida tezi dume linatakiwa kuwa na urefu wa
centimetres 2.5 ukilipima kwa kupitia njia ya Haja kubwa Kwa kitaalamu per
rectal examination. Na vile vile linatakiwa liwe laini na lililo free bila
kujishikia sehemu yeyote. Kwa minajiri hiyo basi njia Rahisi na inayotumika
kwenye nchi maskini ni hiyo ya kufanya PR. Kidole ingawaje kulingana ma
technologia ya kisasa kuna njia zingine zitatumika I kiwepo urinoscope ambayo
kifaa chenye kamera kinaingizwa kwenye njia ya mkojo kwenda kuangalia hilo tezi
dume.
Kwenye kisababishi cha kwanza ni umri cha pili bado kuna
mkanganyiko kutoka kwa wataalamu wengine wanasema ukifanya sana ngono celi za
hili tezi zinakuwa kwa vile linakuwa na kazi kubwa sana kwenye kuzalisha
Shahawa kwa hiyo linaongezeka. Wengine wanasema ukifanya sana unapunguza manii.
Ingawaje hata usipofanya huwa wanaume wengi wanapata njozi pevu na kushusha
mzigo
Sasa basi kwa Tanzania kwa sasa ni kama kuna kampeni ya
kupima tezi dume na kama nilivyoeleza hapo juu njia rahisi na ya gharama nafuu
ni hiyo ya PR kidole ndio maana tunaambiwa wanaume tusiogope kidole.
Tezi dume likikua kuzidi ukubwa wake unaotakiwa linaziba
njia ya kutolea mkojo kwani lipo kwenye shingo ya njia ya mkojo. Mkojo ni sumu
kali sana mwilini. Kwanza kibofu kikikijaa mkojo kinauma sana maumivu makali
sana. Na mkojo ukiendelea kubakii mwilini utarudi kwenye figo them mwilini na
kumsababishia mtu sumu kali uraemia.
No comments:
Post a Comment