Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (TAMISEMI), Mh. George Simbachawene
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (TAMISEMI), Mh. George Simbachawene amemvua madaraka Mkurugenzi Mtendaji
wa Manispaa ya Dodoma, Bw. Augustino Kalinga kufuatia kuruhusu ofisi yake
kuwachangisha wazazi michango ambayo serikali imezuia katika kutoa elimu ya
msingi bila malipo.
Mh. Simbachawene amefikia uamuzi huo leo mjini Dodoma wakati
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatua zilizochukuliwa na serikali
baada ya kugundua kuwa manispaa ya Dodoma imesambaza barua kwa walimu wakuu wa
shule za
msingi ambazo zimeagiza kuwatoza wazazi michango ya maji, umeme na
mlinzi ambayo imekatazwa na serikali.
Amesema kuwa Bw. Kalinga amevuliwa madaraka yake baada ya
kubainika kuwa ameshindwa kuwasimamia watumishi walio chini yake hadi
kusababisha kuandika barua na kusambaza kwa walimu wakuu wa shule za msingi
katika manispaa ya Dodoma ambayo inatofautiana na maelezo ya serikali yaliyopo
kwenye mwongozo.
Aidha, amebainisha kuwa katika mwongozo wa elimu ya msingi
uliotolewa na serikali unafafanua majukumu ya wazazi na walezi ambayo
wanatakiwa kuyafanya kuwa ni pamoja na sare za shule, vifaa vya michezo na vya
kujifunzia pamoja na matibabu na chakula.
No comments:
Post a Comment