Na Woinde Shizza,Arusha
Bendi mpya ya mziki wa dance ijulikanayo kwa jina
Filomena music Band ambayo makazi yake ni mkoani Kilimanjaro
inatarajia kuwapagawisha wakazi wa jiji la arusha na vitongoji vyake
ndani ya usiku wa wapendanao (valentine day).
Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa
mkurugenzi wa bendi hiyo Swaumu Kileo alisema kuwa bendi hiyo inatarajia kutua
jijini Arusha kwa kishindo kwa ajili ya kuitambulisha rasmi bendi hiyo kwa
wakazi wa jiji la arusha pamoja na kuwapa
burudani ya nguvu wakazi wa jiji hilo ambapo alibainisha kuwa burudani watakayo itoa
itakuwa ya kihistori na aijawai kutokea.
Alisema kuwa hii ni mara ya kwanza kwa bendi hii kufanya show ndani ya jiji hili la Arusha kwa hivyo wanaimani wakazi wa jiji hili na vitongoji vyake wataipokea kwa furaha na wataikubali kwakuwa hii ndio bendi ya kwanza kubwa iliopo kanda ya kaskazini.
"ujio huu wa filomena bendi utakuwa ni wakihistoria kwani kwanza ni bendi kutoka mikoa hii hii ya kanda ya kaskazini pia ipo nyumbani kwaiyo ninaimani watafurahi na wakazi wa jiji la arusha na vitongoji vyake wajitokeze kushuhudia bendi hii kwani hii ndio bendi yao ya nyumbani “alisema Swaumu
Aidha alibainisha kuwa katika siku hii ya valentine day wameiandaa maalumu kwa ajili ya kuwaonyesha
washabiki wao kuwa wanawajali hivyo watatumia siku hiyo kuwatambulisha
washabiki wa mziki huu wa dance nyimbo za bendi hiyo ambapo pia alisema watawaonyesha staili
nyingi mpya ambazo azijachezwa na bendi zingine hapa nchini ikiwa ni
pamoja na kuonyesha jinsi kila mtu
anavyotakiwa kutingisha yakwake.
Aidha alibainisha kuwa show hiyo itafanyika ndani ya ukumbi wa milestone garden uliopo jijini hapa huku akibainisha kuwa kwa upande wa viingilio V.I.P watalipa shilingi 20000 huku kawaida wakilipa shilingi 10000 kwa kila mmoja na kusema kuwa kwa wapenzi watakao pendeza kuliko wote wataondoka na bonge la zawadi .
kwa upande wa kiongozi wa bendi hiyo sety Mbeki alisema kuwa timu yake yote imejipanga vyema kuwapa burudani ya nguvu wakazi wa Arusha na kuwapa staili mpya ikiwemo ile ya kila mtu atingishe yakwake ambapo alisema kuwa wameiboresha na imekuwa ya kiufasaha zaidi na ina vinjonjo vingi zaidi ,staili tamu pamoja na maneno matamu.
kwa upande wa kiongozi wa bendi hiyo sety Mbeki alisema kuwa timu yake yote imejipanga vyema kuwapa burudani ya nguvu wakazi wa Arusha na kuwapa staili mpya ikiwemo ile ya kila mtu atingishe yakwake ambapo alisema kuwa wameiboresha na imekuwa ya kiufasaha zaidi na ina vinjonjo vingi zaidi ,staili tamu pamoja na maneno matamu.
Alisema kuwa lengolao kubwa la kufanya onyesho hili ndani ya jiji la arusha ni pamoja kujitambulisha kwa wakazi wa la arusha na kuwaambia wasio wapweke tena kwani wamepata bendi mpya kutoka nyumbani kwao bendi ambayo ni yao inatoka ndani ya kanda yao na ni watoto wa o.
Aliwasihi wakazi wa jiji la arusha na kanda ya kaskazini kwa
ujumla kuwapokea kwa mikon o miwili na kuwapa ushirikiano ili waendelee kuwapa
burudani zaidi.
No comments:
Post a Comment