Picha zinazoonesha akiwa katika harakati za kupanda mlima huo na alipofika kwenye kilele hicho.
Mlima Kilimanjaro.
Tanzania yamuingiza mwanamke
kikongwe kwenye Kitabu cha kumbukumbu za Guinness baada ya kupanda
mlima Kilimanjaro ambao ni mrefu kuliko yote Barani Afrika.
Kwa mujibu wa mtandao wa
Guinness uliochapisha habari hiyo hivi karibuni ulimwelezea Mwanamke
huyo aliyefahamika kwa jina la Angela Verobeva (86) anakuwa wa kwanza
kupanda Mlima Kilimanjaro wenye urefu wa (5,895 m; 19340 ft).
Angela Vorobeva amezaliwa
Februari 4, 1929. Amefikia kilele cha Mlima Kilimanjaro, mnamo Oktoba
29 mwaka 2015. Hata hivyo taarifa zake zimechapishwa mwaka huu 2016
ambapo kwenye taarifa hiyo inaelezea kuwa rekodi yake inaweza kubadilika
endapo kikongwe mwingine anaweza kutokea.
Wakati wa upandaji wa mlima
huo, Kikongwe huyo alikuwa na kundi la msafara na kupitia lango la
Londorossi (2,360 m) mnamo 23 Oktoba 2015 na kufika kelele cha Uhuru
Peak (5,895 m) wakati wa mchana siku ya saba (29 Oktoba 2015) ya safari
yao nzima.
Kundi hilo lilishuka juu ya kilele hicho cha Uhuru, 30 Oktoba 2015, kupitia lango la Mweka (1,640 m). Mtandao
huu Modewji unatoa rai kwa wananchi wa Tanzania kutumia nafasi hii
kupanda mlima huo mrefu Barani Afrika kumbukumbu ya kihistoria.
Habari hizi zimeandaliwa na Andrew Chale,modewjiblog.com
No comments:
Post a Comment