LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania bara mzunguko wa 17 unatarajiwa
kuendelea kesho Jumatano kwa michezo sita kuchezwa katika viwanja mbalimbali,
huku kila timu ikisaka pointi tatu muhimu kwenye msimamo wa ligi hiyo.
Kesho Jumatano, Simba SC watakua wenyeji wa maafande wa
Mgambo Shooting kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, JKT Ruvu
watawakaribisha Mbeya City katika uwanja wa kumbukumu ya Karume Ilala, huku
Mtibwa Sugar wakicheza dhidi ya Toto Africans katika uwanja wa Manungu –
Turiani.
Jijini Mbeya, Tanzania Prisons watakua wenyeji wa vinara wa
ligi hiyo Young Africans katika uwanja wa Sokoine, Wana kimanumanu African
Sports watacheza dhidi ya Mwadui FC uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, huku
wakata miwa wa Kagera Sugar wakiwakaribisha Majimaji FC katika uwanja wa
Kamabarage mjini Shinyanga.
Alhamisi ligi hiyo itaendelea kwa kuchezwa mchezo mmoja tu,
Wagosi wa Kaya Coastal Union watawakaribisha Ndanda FC katika uwanja wa
Mkwakwani jijini Tanga.
Michezo ya viporo ya Azam FC imepangiwa ratiba, mchezo dhidi
ya Tanzania Prisons utachezwa Februari 24 uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, huku
mchezo dhidi ya Stand United ukichezwa Machi 16 katika uwanja wa Azam Complex.
No comments:
Post a Comment