Pages

Monday, February 15, 2016

LUNDENGA ASIKITISHWA NA MANENO YA MTANDAONI KUHUSU HOYCE TEMU (AUDIO)‏

Hashim Lundenga
Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga (pichani) amezungumza na Modewjiblog kuhusu habari zilizosambaa katika mitandao ya kijamii kumhusu Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu.
Lundenga amesema kuwa yeye kama Mwenyekiti wa kamati ya Miss Tanzania na Mtanzania wa kawaida amesikitishwa na maneno hayo na kuwa hayapendezi kusemwa kwa mtu kama Hoyce ambaye amejitoa kusaidia jamii.
Alisema kuwa anashangazwa na mtu ambaye amekuwa akiandika maneno hayo mtandaoni kwani hawakuwa na utofauti wowote na kilichokifanya ni kumuandika Hoyce ambaye hakuhusika katika ugomvi uliokuwepo baina ya mtu huyo na mdogo wake Hoyce, Rachel.
 
“Nimesikia habari hizo kumhusu Hoyce kwa kweli nimesikitishwa sana, sio jambo zuri ambalo amelifanya huyo aliyemuandika,” alisema Lundenga.
Hata hivyo mwenyekiti huyo aliwataka watumiaji wa mtandao kuwa na matumizi mazuri ya mtandao ili kuzidi kuifanya mitandao ya kijamii kuwa sehemu salama kwa ndugu na marafiki kuwasiliana.
Zaidi unaweza kusikiliza maneno ya Lundenga hapa chini.

No comments:

Post a Comment