ke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiweka saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge,
Kigamboni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akikabidhiwa taarifa Bw. Ojuku Mgedzi, Mkuu wa Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, Kigamboni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana kwa furaha na wakaazi wa Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, Kigambo ni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
PICHA NA IKULU
Na Magreth Kinabo –MAELEZO
MKE wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Janeth Magufuli ameziomba na kuzimahamasisha taasisi za Serikali na zisizo za Serikali kushirikiana na Serikali kutatua changamoto mbalimbali zinazozikabili Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu Wasiojiweza kijulikanacho kwa jina la Nunge,viwemo vingine.
Aidha alisema vituo hivyo jumla vipo 17, katika maeneo mbalimbali nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mama Magufuli wakati alipotembelea makazi hayo yaliyoko Kigamboni eneo la Vijibweni jijini Dares Salaam, ambapo alisema changamoto wanazokabiliana nazo amezisikia na na aliwaahidi kuwa atashirikiana na wadau wote kuzitafutia majibu yake.
Mama Magufuli alizitaja baadhi ya changamoto hizo, ni kuwa uchakavu wa miundombinu, uhaba wa rasilimali fedha na watu, pamoja na maslahi duni ya watoa huduma, upungufu wa vitendea kazi na huduma za jamii, pamoja na uvamizi wa eneo la kituo.
Aidha Mama Magufuli alimwomba Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema kulishughulikia taizo la uvamizi wa eneo hilo na kulitafutia ufumbuzi.
“ Natumainni zawadi tuliyoileta ni ndogo na haiwezi kumaliza matatizo yote mliyonayo. Lakini ni matumaini yangu kuwa zawadi hii inaweza kuwa chachu ya kuhamsha hamasa ya watu na vikundi vingine kujitoa kusaidia watu wasiojiweza. Ni imani yangu kuwa endapo watu wote tutajitoa kwa dhati tutaweza kuwahudumia wazee na watu wasiojiweza na hivyo kuwapunguzia makali ya maisha.
No comments:
Post a Comment